Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani akizungumza na wadau jana wakati wa dhifa yakukabidhi Mradi wa malezi kwa makuzi
Picha na Tiganya Vincent
NA:TIGANYA VINCENT – RS,TABORA.
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema malezi na makuzi katika familia linapaswa kuwa ni la wazazi wote wawili tangu mtoto akiwa tumboni lengo la kumjenga kiakili.
Alisema hatua hiyo itasaidia kuwa na vijana na wazee wenye upendo na ushirikiano nyakati zote.
Balozi Dkt. Batilda alitoa kauli hiyo jana wakati wa dhifa yakukabidhi Mradi wa malezi kwa makuzi
Alisema malezi yamesababisha kukosekana kwa upendo kwa baadhi ya vijana kushindwa kuwatunza wazazi wao wanapokuwa wazee na wakati mwingine kudiri kuwakatisha masiaha yao ili waweze kurithi mali.
Balozi Dkt. Batilda alisema malezi ya mtoto yanaanza siku mama anapopata ujauzito kwa kumweleza maeneo mazuri yakiwemo ya kumfundisha kuepnda dini ilia je awe raia mwema.
Alisema kwamba kwa sasa, Malezi na makuzi imejumuishwa katika miongozo mbali mbali ya utoaji huduma za afya hivyo ni wajibu wa wadau muhimu wa afya kwenda kutekeleza miongozo ya kitaifa ya utoaji wa huduma za afya , ikiwemo Malezi kwa makuzi na ustawi wa jamii.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba Serikali imedhamiria kuendeleza Mpango wa malezi na Makuzi hasa kwa kuziagiza halmashauri zote zitaendeleza ili kuepusha watoto na udumavu na kupata lishe bora.
Alisema sanjari na hilo mtoto anapaswa kupata lishe nzuri tangu awali ili kukuza akili yake.
Balozi Dkt. Batilda alisema kufuatia umuhimu wa lishe bora kwa ajili ya makuzi ya mtoto amewaagiza Wakuu wote wa Wilaya ya Mkoa wa Tabora kuhakikisha wanzisimamia Halmashauri ziwe zinatenga shilingi 1,000/= kwa ajili ya watoto kupata lishe.
“Nasisitiza tena kuendelea kutenga Kiasi cha Tsh. 1000/= kwa kila mtoto chini ya miaka 5 kama tulivyoagizwa na serikali” alisema Balozi Dkt Buriani.
|