Home LOCAL RAIS MHE. SAMIA AONGOZA VIONGOZI KUAGA MWILI WA MAREHEMU MZEE CHRISANT MZINDAKAYA...

RAIS MHE. SAMIA AONGOZA VIONGOZI KUAGA MWILI WA MAREHEMU MZEE CHRISANT MZINDAKAYA KATIKA KANISA KATOLIKI LA ST. PETER DAR.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho katika Jeneza lenye mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Marehemu Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya mara baada ya Misa ya kumuombea Marehemu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay mkoani Dar es Salaam leo tarehe 09 Juni 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Misa ya kumuombea Marehemu Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay mkoani Dar es Salaam leo tarehe 09 Juni, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay mkoani Dar es Salaam mara baada ya kutoa Heshima za mwisho katika Jeneza lenye mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Marehemu Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya leo tarehe 09 Juni, 2021.

Previous articleWAZIRI GWAJIMA: ‘ JUKUMU LA KUWALEA NA KUWALINDA WATOTO NI LA FAMILIA NA JAMII’
Next articleMAJALIWA ATEMBELEA BANDA LA TET KATIKA KONGAMANO LA MIAKA 50 LA ELIMU YA WATU WAZIMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here