Home Uncategorized NEEC YAWAITA WADAU KUJADILI NAMNA WANANCHI KUSHIRIKI MIRADI YA MAENDELEO.

NEEC YAWAITA WADAU KUJADILI NAMNA WANANCHI KUSHIRIKI MIRADI YA MAENDELEO.

DAR ES SALAAM.

Katibu Mtendaji wa Baraza la uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) Beng’i Issa leo Juni 1 amezindua washa ya wadau kujadiliana na kupitia rasimu ya mkakati wa utekelezaji wa ushiriki wa wanachi katika miradi ya kimkakati katika Sekta mbalimbali Nchini.

Akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki washa hiyo katika Ukumbi wa Mount Meru uliopo Benki Kuu, Dar es Salaam ambapo Mgeni alikuwa mgeni rasmi amesema kuwa  wadau mbali mbali wamehusika ili kuhakikisha wanatoa michango na hoja ambazo zitasaidia Wananchi waweze kushiriki vilivyo kwenye sekta hiyo.

Baadhi ya wadau au Taasisi zilizoshiriki ni pamoja na TPDC, PURA, GGML, Tume ya Madini, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Kilimo, VETA, NBS, UDSM, TANESCO, IFM, CBE, ERB.

Akifungua warsha hiyo Bibi Beng’i Issa aliwashukuru wadau wote waliojitokeza katika warsha hiyo muhimu ambayo itasaidia kutengeneza Mkakati wenye manufaa kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla.

Aliongeza kuwa sekta ya Uziduaji ni sekta ambayo inaweza kumuinua Mwananchi Kiuchumi kwa kuajiriwa au ununuaji wa vifaa vya ndani na huduma.

“Sote tunafahamu kuwa nchi yetu imejaaliwa rasilimali nyingi ikiwemo madini pamoja na gesi ambayo imegundulika katika kina kirefu cha Bahari na nchi kavu, ili Wananchi waweze kunufaika na rasilimali hizi Serikali imefanya jitihada kubwa kuhakikisha inatunga sera, sheria kanuni na miongozo mbalimbali ikiwemo sera ya nishati, 2015, sheria ya mafuta, 2015,  sheria ya madini, 2010 na marekebisho yake, 2017 na kanuni za Local content kwenye sekta ya mafuta na madini.” Alieleza Katibu Mtendaji.

Aliongeza kuwa sera na sheria zimeanisha Ushiriki wa Watanzania katika maeneo ya ajira, ununuzi wa bidhaa na huduma, ujengaji uwezo, uhaulishaji wa teknolojia, utafiti na huduma kwa jamii (Corporate Social Responsibility).

“Tanzania kwa sasa inatekeleza miradi mingi ya kimkakati ambayo imesaidia kuwapa ajira Watanzania wengi na fursa hivyo tuna wajibu wa kuwa na Mkakati mzuri na wenye maslahi mapana.” Alisisitiza Katibu Mtendaji.

Katibu Mtendaji aliishukuru benki ya AfDB kwa kudhamini warsha hiyo lakini pia Shirika la TPDC kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika uandaaji hadi utekelezaji wa warsha.
Previous articleWAZIRI UMMY ATANGAZA WANAFUNZI 148,127 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI 2021.
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.TANO JUNI 2-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here