Home LOCAL MEYA JIJI LA DAR ES SALAAM AFUNGUA SEMA PAMOJA NA MAONESHO YA...

MEYA JIJI LA DAR ES SALAAM AFUNGUA SEMA PAMOJA NA MAONESHO YA BIDHAA ZA WAJASIRIAMALI.

Na: Juma Mizungu, PuguMedia Online

Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe Omary Kumbilamoto amefungua Semina ya Wajasiriliamali pamoja na Maonesho ya bidhaa za Wajasiriliamali yaliyo andaliwa na Taasisi ya Tuamke pamoja katika Ukumbi wa Check Point Pugu Jijini Dar es salaam.

Mafunzo hayo ambayo yamedumu kwa muda siku moja yalikuwa na malengo ya kuwaongezea uwezo Wajasiriliamali wadogo katika kutengeneza bidhaa pamoja na kutafuta masoko ya ndani pamoja na ya nje.

Mhe. Kumbilamoto ameipongeza Taasisi ya tuamke pamoja ikiongozwa na Mkurugenzi wake Bi Nasra kwa kuandaa mafunzo hayo pamoja na maonesha ya bidhaa zao kwani zimewafanya Wajasiriliamali kuendelea kuongeza wigo mpana wa biashara zao.

Mhe. Kumbilamoto amewataka Wajasiriliamali wote kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kuitumia vyema mikopo inayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kupitia Halmashauri ya Jiji katika kukuza uchumi wa vikundi vyao vya Ujasiriamali lakini pia kurejesha mikopo hiyo ili kutoa fursa kwa watu wengine kukopa.

Mwisho Mhe. Kumbilamoto ametembelea Meza za maonesho ya bidhaa za Wajasiriliamali hao pamoja na kutoa vyeti vya kushiriki katika Semina hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here