Home LOCAL MBUNGE ALIYEVAA SURUALI YA KUBANA AONDOLEWA BUNGENI

MBUNGE ALIYEVAA SURUALI YA KUBANA AONDOLEWA BUNGENI

BUNGENI, DODOMA.

Mbunge wa Momba Condester Michael Sichalwe ametolewa ndani ya ukumbi wa bunge ili akabadilishe mavazi yake baada ya mbunge wa Nyangw’ale, Hussein Nassor Amar kuomba muongozo wa Spika kuwa kuna baadhi ya wabunge wamevaa mavazi yasio na maadili.

Spika alimtaka mbunge Hussein Nassor Amar kumtaja mmoja ambaye amemuona ndipo alipomtaja Mbunge wa Momba Condester Michael Sichalwe ambapo Spika Ndugai alimtaka atoke ndani ya ukumbi wa bunge ili akabadilishe mavazi yake.

“Spika nasimama kwa kanuni ya  70 inayohusu mavazi ya staha kwa wabunge, kanuni imeeleza  wazi kuhusu mavazi hayo na kwa akina dada lakini humu ndani kuna wabunge wamevaa nguo ambazo hazina staha,” Amar.

Spika Ndugai alimpa nafasi Mbunge huyo kumtaja mwenzake  aliyevaa mavazi ambayo hayakuwa na staha ili iwe mfano.

“Mbunge huyo yuko hapo katika mkono wangu wa kulia, amevalia tisheti  lakini naomba umuite mbele uone suruali aliyovaa namna ilivyobana, amevaa miwani,”  Amar.

Previous articleMKUU WA MKOA MARA AFUNGUA MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU KITAIFA, APONGEZA MCHANGO WA WADAU WA ELIMU
Next articleWATAALEM SEKTA YA MANUNUZI WAASHWA KUWA WAADILIFU.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here