Home LOCAL MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA (TMDA) KUTOA MAJIBU ATHARI ZA VIDONGE...

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA (TMDA) KUTOA MAJIBU ATHARI ZA VIDONGE VYA P2


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Nchini (TMDA), Bw. Adam Fimbo akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) vitambulisho vya wakaguzi vyenye namba maalum wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wakaguzi wapya kutoka Kanda Nane za Mamlaka hiyo, yanayofanyika Kibaha, mkoani Pwani.

Afisa wa Sheri wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), Wakili Bi. Donesta Byarugaba akiwasilisha mada juu ya Sheria ya Dawa na Vifaa tiba Sura 219 kwa wakaguzi wa TMDA wanaoshiriki katika mafunzo maalum ya ukaguzi ya siku Nne, yanayoendelea, Kibaha Pwani.

KIBAHA, PWANI.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Nchini (TMDA), Bw. Adam Fimbo  amesema kuwa, mamlaka hiyo inaendelea kuzifanyia tathimini dawa za kuzuia mimba za dharura vya vidonge (Emergence Contraceptive Pills’) maarufu kama P2 ambapo hivi karibuni wataalam wa afya walisema vinasababisha madhara kwa watumiaji.

Akizungumza mjini hapa kando ya ufunguzi wa mafunzo ya Wakaguzi wapya 59 kutoka Kanda Nane za Mamlaka hiyo nchini, Fimbo alisema kuwa wanataarifa ya uwepo wa matumizi holela wa dawa hizo za P2 na watakapokamilisha wataweka wazi.

Ambapo amebainisha kuwa ,Dawa za uzazi wa mpango hizo zinatumika ili kuzuia mtu kama anapata mimba  ya dharura P2, zinasajiliwa na kudhibitiwa na  TMDA  ikiwemo uingiaji wake, usambazaji wake na matumizi yake kwenye soko.

“Kwa sasa tunafuatilia juu ya matumizi yasiyo sahihi kwa kuzifanyia tathimini ya kina kufahamu kwa nini isitumike inavyopaswa.

“Tunafahamu dawa hizi utumiwa endapo umepewa cheti na Daktari ueze kuitumia kwa inavyotakiwa kama inavyikusudiwa hivyo tutakapokamilisha kubaini ukweli wa kwa nini inatumika isivyofaa tutawataarifu.

Aidha, Fimbo alisema ni kweli kuna taarifa za dawa hiyo kutumika isivyofaa wataalam wapo kazini kuendelea na uchunguzi wake.

Katika kuhakikisha wanaendelea kufanya kazi kwa weredi na ubora katika kukagua dawa, amesema Wakaguzi wote nchi nzima wana namba maalum zilizounganishwa na mifumo ya kisasa ya utambuzi (Codes number) ilikuepuka wakaguzi feki (Vishoka).

“Mkaguzi anapoingia eneo la ukaguzi lazima ajitambulishe na aonyeshe vitambulisho ambavyo ni maalum tumeviandaa. 

Kama atatumia kitambulisbo bandia tutambaini kutokana vinanamba muhim ya utambulisho tukiingia kwenye mifumo yetu na alama ya utambuzi isipokugundua basi wewe ni feki” alisema. Fimbo.

Mafunzo hayo ya siku Nne, yameanza yameanza jana 7 Juni ambapo wakaguzi hao watapatiwa mafunzo mbalimbali ambapo yanatarajiwa kufungwa 10 Juni mwaka huu.

TMDA imeandaa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO)  amabapo mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara kwa wakaguzi na maafisa wa TMDA nchi nzima.

MWISHO.

Previous articleSERIKALI YASISITIZA MIONGOZO YA YA KUJIKINGA NA COVID-19 IZINGATIWE
Next articleRAIS SAMIA AZUNGUMZA NA WANAWAKE WA TANZANIA JIJINI DODOMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here