Home LOCAL MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AZUNGUMZA NA RAIS NDAYISHIMIYE WA BURUNDI

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AZUNGUMZA NA RAIS NDAYISHIMIYE WA BURUNDI

Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango Ofisini kwake Ikulu Gitega Burundi kwa ajili ya Mazungumzo. Makamu wa Rais  Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amemuwakilisha Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana katika Mji Mkuu wa Serikali Gitega Nchini Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu Gitega Nchini wakati Makamu wa Rais  Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amemuwakilisha Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana katika Mji Mkuu wa Serikali Gitega Nchini Burundi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango, akiagana na Baadhi ya Watumishi wa Taasisi za Serikali ya Burundi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melkior Ndadaye Bujumbura Burundi, alipokuwa akirejea Nchini Baada ya kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana katika Mji Mkuu wa Serikali Gitega Nchini Burundi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here