Home LOCAL MADIWANI WA HALMASHAURI JIJI DAR WAOMBA MAFUNZO

MADIWANI WA HALMASHAURI JIJI DAR WAOMBA MAFUNZO

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akiongoza kikao cha baraza la Madiwani Juni 25/2025.

Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika kikao cha Baraza la  Halmashauri ya Jiji lililovunjwa Juni 25/2021wakati wa kupokea Taarifa ya Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ambapo Jiji lililovunjwa limepata hati yenye mashaka

NA: HERI SHAABAN (ILALA)

BARAZA LA MADIWANI la Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam  wameomba wapatiwe semina mbalimbali kwa ajili ya kuwajengea uwezo katika utekekezaji wa majukumu yao.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam  katika Baraza la madiwani la Halmashauri ya jiji lililovunjwa na Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto wakati wa kupokea taarifa ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ya mwaka 2019/2020 jiji hilo lililovunjwa lilipata hati yenye Mashaka.

Meya  Kumbilamoto alisema siri ya iliyokuwa Halmashauri ya Ilala kupata hati safi mfurulizo kwa kipindi cha miaka mitano MADIWANI wake wamekuwa wakipewa semina mbalimbali na mafunzo kwa ajili ya kuwajengea uwezo ikiwemo pia katika kusimamia miradi ya maendeleo na wamekuwa wakifanya vizuri katika usimamiaji wao.

“Namba madiwangu wangu wote wapate mafunzo ili waweze kuleta maendeleo ya kutosha watekeleze majukumu yao vizuri katika usimamiaji miradi mbalimbali ambayo inapitishwa na halmashauri yao” alisema Kumbilamoto.

Akizungumza hati safi Meya Kumbilamoto alisema kwa kuwa wamepewa hadhi ya Jiji na Serikali watashirikiana vizuri na Madiwani wake Watendaji katika kusimamia mapato na miradi ya maendeleo.

Meya Kumbilamoto akizunhumzia  Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kabla halijavunjwa iliweza kupata hati yenye mashaka, Jiji hilo lilivunjwa tarehe 24/02/2021 na taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ilitoka tarehe 31/03/202. Ili kukamilisha utaratibu wa kujadili taarifa ya CAG Halmashauri ya Jiji Jipya inawajibika kukamilisha utaratibu huo kupitia vikao vyake.

Baraza la Madiwani limepitia taarifa hiyo na kuelekeza kuwa hoja ambazo hazijafungwa zifanyiwe kazi na kuwasilishwa kwa CAG kwa ajili ya uhakiki. Baraza limemsisitiza CAG kufanya uhakiki wa kina kwa hoja ambazo hazijafungwa kwani zinahusu mali ambazo zimegawanywa katika Halmashauri mbalimbali ikiwemo hii ya Jiji la Dar es salaam.

Hoja zilizowasilishwa ni 26, Hoja zilizofungwa ni 6 sawa na asilimia 23%, Hoja zinazo endelea kufanyiwa kazi ni 20  sawa na asilimia 77%. Ikumbukwe kuwa hoja hizi ni za iliyokuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam lililovunjwa. Hivyo ushauri wowote na maelekezo ya CAG yatahusu mamlaka iliyopitia na sii Halmashauri ya Jiji Jipya.

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here