Home LOCAL JAMII YAASWA KUTUNZA MAZINGIRA KWA KUTUMIA NISHATI MBADALA ILI KUOKOA MFUMO WA...

JAMII YAASWA KUTUNZA MAZINGIRA KWA KUTUMIA NISHATI MBADALA ILI KUOKOA MFUMO WA IKOLOJIA

 

Mhandisi Mwandamizi wa Baraza la Taifa la usimamizi wa mazingira (NEMC) kanda ya Kaskazini Nancy Nyenga akiobgea na waandishi wa Habari Mkoani Arusha.

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Katika kuelekea kilele cha siku ya mazingira Duniani inayotarajiwa kufanyika June 5 imeelezwa kuwa hakuna dunia nyingine zaidi ya hii hivyo ni jukumu la kila mtu kutunza mazingira kwa ustawi wa afya na maendeleo endelevu kwa kutumia nishati mbadala ili kuokoa mfumo ya ikolojia .

Hayo yalielezwa na mhandisi mwandamizi wa baraza la taifa la usimamizi wa mazingira (NEMC) kanda ya Kaskazini Mhandisi Nancy Nyenga wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa katika utunzaji huo ni vyema matumizi ya nishati mbadala ikatumika hasa katika utunzaji wa mfumo wa ikolojia.

Mhandisi Nyenga alisema kuwa nishati mbadala ni nishati kutoka vyanzo vya asili kama vile mwanga wa jua, upepo, joto la ardhini, mawimbi, maji, biogesi, kuni na aina nyingine za biomasi au nishati tofauti na fueli za kisukuku(fossilfuel} ambayo yanayatoka kwenye vyanzo vya makaa yam awe, gesi asilia au mafuta ya petroli.

“Hizi zote zinaendelea kupungua kadiri zinavyoendelea kutumika na hata gesi inaweza kutumika kama mbadala wa matumizi ya mkaa kwani ni rafiki kwa mazingira yetu na faida ya utumiaji wa nishati mbadala ni pamoja na kutotoa uzalishaji wa gesi ya ukaa,” Alisema Eng, Nyenga.

Alifafanua kuwa gesi ya ukaa ni kama vile kaboni dioksaidi na gesi zingine chafu zinazochangia ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya hali ya hewa na ndio sababu kwamba ni muhimu jamii zianze kujibadilisha kutoka kutumia nishati ambazo zinzleta madhara na kuanza kutumia nishati mbadala.

Aidha alisema kuwa mfumo wa ikolojia asili na bioanuwai unatoa kwa kiasi kikubwa mahitaji muhimu kama vile chakula kutokana na kilimo na uvuvi, maji, motisha na ustawi wa maisha bora, mapato kutokana na shughuli za utalii pamoja na faida zisizo za moja kwa moja kama vile kuzuia mafuriko na magonjwa. 

Alisema kuwa vichecheo ambavyo ni vya moja kwa moja ni pamoja na mabadiliko ya matumizi ya ardhi kama vile maendeleo ya kilimo na viwanda, sayansi na teknolojia kuwa na matumizi ya kemikali yasiyozingatia taratibu na uhifadhi wa ikolojia na utumiaji wa teknojia usio rafiki kwa mazingira , uwekezaji usiozingatia uhifadhi wa mdhingira pamoja na  ongezeko la watu.

Sambamba na hayo pia alieleza kuwa mbinu za kukabiliana na uharibifu huo ni pamoja na upandaji wa miti ya asili karibu na vyanzo vya maji na kutokufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo, matumizi mazuri ya uandaaji wa mashamba kwaajili ya kilimo cha kisasa, jamii kuwa na makazi ya kudumu pamoja na kuwa na mfumo wa matumizi bora ya ardhi.

Alieleza nji nyingine ni matumizi ya kemikali kwa kuzingatia utaratibu na teknolojia, matumizya nishati jadidifu, kudhibiti mimea vamizi, kudhibiti ongezeko la watu, kudhibiti biashara haramu ya mimea na wanyama, wa huduma za mfumo wa ikolojia pamoja na kuipa kipaumbele uhifadi wa ikolijia na mazingira kwa ujumla.

Hata hivyo uharibifu wa mfumo wa ikolojia unaweza kuleta mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuwa na mvua zisizo na mpangilio,ongezeko la joto, mvua kubwa kupita kiasi au kukosekana kwa mvua, kuongezeka kwa kina cha maji kwenye bahari na maziwa, kuzuka kwa magonjwa, kupungua kwa uzalishaji wa mazao, kupungua kwa ubora wa maji kwenye mito pamoja na kupungua kwa uoto wa asili.

Previous articleWANANCHI KATA YA MILO WAOMBA ELIMU YA UWATIKAJI.
Next articleKARIBU USOME HABARI MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 3-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here