NA: NAMMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Kufuatia utumiaji wa kuni na mkaa kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa ikolojia ya dunia Shirika lisilo la kiserikali Dorcas aid international limekuja na njia ya kutumia nishati mbadala ya jiko linaloitwa mimi moto linalopika kwa muda mfupi kwa kutumia mkaa mbadala unaotengenezwa kwa kutumia masalia ya mimea.
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika halmashauri ya Meru mkurugenzi wa shirika hilo Lilian Michael alisema kuwa nia ya shirika hilo ni kusaidia watu walio katika mazingira magumu ambapo kupitia jiko hilo wameweza kuwanufaisha akina mama ambao pamoja na ikolojia kuharibika kutokana na matumizi ya mkaa na kuni ambayo pia husababisha uharibifu wa mazingira kwa miti kukatwa wamekuwa wakipatashida za kiafya kutokana na moshi.
“Akina mama wamekuwa wakipata shida sana kwenye habari ya kupika kwasababu ya kutumia kuni na mkaa unaofanya moshi kuadhiri afya zao ikiwemo macho na upumuaji, lakini pia kuharibu mazingira kwa kutumia nishati hizo jambo ambalo limetufanya sisi Dorcas kuja na wazo hili la jiko ambalo mtu anapika kwa muda mfupi lakini pia halina moshi kwa kutumia mkaa mbadala unaotengenezwa kwa kutumia masalia ya mimea,”Alisema Bi Lilian Michael.
Alisema kuwa Dorcas wanakusanya masalia ya mimea na kutengeneza mkaa huo unaoitwa Pellet ambao unatumika kwenye jiko hilo la Mimi Moto na kwasasa wana wateja zaidi ya 500 kwa wilaya ya Meru na akina mama wameanza kufurahia matumizi ya jiko hilo.
Alifafanua kuwa jiko hilo mtu anaweza kupikia sehemu yoyote ya nyumba yake kwani halina moshi ambapo katika kuadhimisha wiki ya mazingira wameona ni kuanza kuieleza jamii kuwa matumizi ya mkaa sio sahihi hivyo waanze kupunguza kwani wanapohifadhi misitu wanahifadhi mambo mengi.
“Misitu inasaidia kilimo, mazingira na maji lakini pia inatusaidia tupata hewa safi kwahiyo sisi tumeamua kuhifadhi misitu kwakutengeneza haya majiko kama nishati mbadala kwa wakati huu kwani uharibifu unaofanyika leo unaleta athari sasa na kwa vizazi vya baadae,”Alisema.
Aliendelea kusema kuwa matokeo yanayoonekana sasa hivi ya mabadiliko ya hali ya hewa ni kutokana na uharibifu uliofanyika lakini jamii ikianza kubadilika kwanzia sasa watawabalisha na wengine na baadae kujikuta wamefanya uhifadhi mzuri wa mazingira na hali ya hewa kurudi kama kawaida hali itayomnufaisha kila mtu wakiwemo wakulima.
Aidaha alisema kuwa kwa sas wapo wilayani Arumeru lakini wana mikakati ya kufika nchi nzima kwani hawapo kwaajili ya kupata faida bali wanapeleka wazo hilo kwenye jamii na kuwawezesha wajasiriamali ambao wataweza kuchukua teknolojia hiyo ili waweze kujikita katika uchakataji wa mkaa huo mbadala na wengine kusambaza majiko hayo hali itayofanya watu wengi kupata kwa wakati na kuweza kutumia .
Mmoja wa wanufaika wa jiko hilo Catherin Pallangyokutoka katika kijiji cha Kwaugoro kata ya Maroroni alisema kuwa jiko hilo limewasaidia kwani walikuwa wanateseka na moshi kwa kutumia kuni na mkaa ambapo umewarahisishia kuweza kupika kwa muda mfupihuku wakiendelea kufanya shughuli zingine tofauti na awali ambapo walikuwa wakitumia kuni walikuwa wakilazimika kukaa mahali hapo kwaajili ya kuchochea.
“Mazingira yetu kwasasa yamekuwa mazuri kwali tulikuwa tukikata miti kwajili ya kuni jambo ambalo hatulifanyi tena, tumeona ni rahisi kwetu kwani jiko hili linawaka na linaturahisishia maisha sula la moshi lililokuwa linatuumiza macho sasa tumelisahau na tunaishi maisha mazuri,”Alisema Catherin.
Ni