Home LOCAL DKT. KABATI AHOJI ABIRIA WANAOATHIRIKA NA AJALI KUTOLIPWA FIDIA ZAO.

DKT. KABATI AHOJI ABIRIA WANAOATHIRIKA NA AJALI KUTOLIPWA FIDIA ZAO.

DODOMA.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM), Dkt. Ritta Kabati ameitaka serikali kuchukua hatua kuhusu changamoto ya waathirika wa matukio ya ajali kukosa malipo ya fidia yatokanayo na Bima zilizokatwa na vyombo vya usafiri wanavyovitumia.

Kabati ameyasema hayo leo bungeni, Jijini Dodoma katika swali lake la msingi lililouliza je, ni chombo gani kinasaidia abiria kupata haki pindi anapopata ajali akiwa safarini lililoelekezwa wizara ya mambo ya ndani ya Nchi na kujibiwa na Naibu waziri, Khamis Hamza Chilo.

Kabati ameitaka serikali kuelekeza mkakati wao kuhusu kutoa elimu kwa wananchi ambao wengi wao huwa wahanga wa ajali kwa kupoteza viungo au kupoteza maisha bila kujua namna ya kupata haki yako ya fidia.

Katika majibu yake ya msingi, Naibu Waziri, Khamis Hamza Chilo, amesema ni haki ya mtu, watu au chombo kilichopata ajali kupata haki  yako ya msimgi ya fidia kwa taasisi au kampuni za bima walizokata kwa ajili ya kulipwa fidia kulingana na ukubwa wa madhara kulingana na taarifa za jeshi la Polisi na madaktari.

Chilo amekiri kuwepo kwa changamoto ya namna bora wanayoweza kuitumia abiria au watumiaji wa usafiri walioathirika na ajali kuandika barua na maelezo ili wapatiwe fidia zao.

Waziri Chilo ametaja changamoto ya kuchelewa kwa upelelezi wa matukio ya ajali ili kusaidia upatikanaji wa fidia kwa vyombo vya usafiri vilivyojiunga na huduma ya Bima pamoja na watu ambao wamekuwa wahanga.

Chilo amelitaka jeshi la polisi kukamilisha kwa haraka upelelezi unaohusisha masuala ya ajali ili iweze kuwasaidia wananchi wanaokuwa wahanga wa ajali kupata fidia kwa wakati. 

Katika hatua nyingine, Naibu waziri Chilo amempongeza mbunge Ritta Kabati kwa ujenzi wa kituo cha polisi kilichopo Semtema, Kata ya Kihesa katika manispaa ya Iringa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here