Home ENTERTAINMENTS DAVIDO KUKNUKISHA EAST AFRKA MUBASHARA JUNE 8

DAVIDO KUKNUKISHA EAST AFRKA MUBASHARA JUNE 8

 

 Na: MWANDISHI WETU, DAR.
Promote mkongwe wa muziki nchin Dickson Mkama, ambaye ni mmiliki wa kampuni ya DMK Global Concept ameanda tamasha la muziki mbashara ambalo litamhusiasha msanii Davido kutoka Niageria.

DMK Global Concept, imekuwa ikiwachukua wasanii mbalimbali hapa nchini kuwapeleka kufanya shoo nje ya Afrika miongoni  mwa wasanii hao ni Nasibu Abduli ‘Diamond’ na Faustine Chales ‘Nandy’ ambao walipata frusa ya kufanya kazi na kampuni hiyo nchin Marekani.

Akizungumza na wandishi wa habari DMK, amesema ameandaa tamasha na msanii Davido ambalo litaruka June 18, mubasha kupitia mtandao wa Shuruti.Com, litaonekana dunia nzima kwa gharama nafuu.

Tamasha hili tumelipatia jina la Davido Global Unity,  litafanyika nchini Nigeria lakini hakutakuwa na mashabiki kama ilivyo zoeleka hivyo nchi zote zita tazama kwa gharama ya dola 5 kupitia mtandao wa Shuruti.Com” anasema DMK.

Aliongeza kuwa shoo kama hii imekuwa ikifanyika bara la Ulaya ila kwa ukanda wa East Afrika hii itakuwa ya kwanza pia itahusisha wasanii kutoka nchi tofauti ikiwemo na Tanzania.

“Huu ni mwanzo tutakuwa tunafanya tamasha hili mara kwa mara kila msanii atakaye pata frusa hii shoo itafanyika nchini kwake na Tanzani ni miongoni mwa nchi hizo ndiyo sababu uzinduzi umefanyika hapa.”
Previous articleWAZIRI GWAJIMA AKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO WA MFUKO WA AFYA WA PAMOJA
Next articleMEYA KUMBILAMOTO AKAGUA UJENZI WA TENKI LA MAJI MACHINJIO YA VINGUNGUTI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here