Afisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Methusela Mahona akimkabidhi cheti cha usajili wa jina la biashara Jacqueline Said Sevury, baada ya kusajili kwa njia ya mtandao katika banda la BRELA, wakati wa kongamano la Vijana lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo, kongamano hili lillilohusu Ujasiriamali, Uwekezaji na Maendeleo ya Kiuchumi, lilifanyika tarehe 12 Juni, 2021 katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kitunda Relini Jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Sweetness Madata(kushoto) na Joram Manyika(kulia) wakitoa huduma ya usajili kwa njia ya mtandao kwa vijana walioshiriki Kongamano la Vijana na Maendeleo Benki, lililohusu Ujasiriamali, Uwekezaji na Maendeleo ya Kiuchumi. Kongamano hilo lilifanyika katika Kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), Usharika wa Kitunda Relini tarehe 12 Juni, 2021.