|
Afisa msajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw.Salehe Yahaya, akitoa elimu juu ya namna ya kusajili na umuhimu wa kusajili majina ya biashara na upataji wa leseni kwa njia ya mtandao, katika Mkutano Mkuu wa uzinduzi wa Jumuiya ya Wazee wa Wilaya ya Same (JUWASA) uliofanyika ukumbi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Same. Mkutano huo wa siku moja umefanyika kwa lengo la kuzindua jumuiya hiyo ya wazee, ambayo ilizinduliwa rasmi na Katibu tawala wa Wilaya ya Same Bw. Sospeter Magonera. |
|
Katibu tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Mhe.Sospeter Magonera, akizungumza na Jumuiya ya Wazee wa wilaya ya Same (JUWASA), wakati wa uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Same. kutoka kulia ni Bw. Paul Peter Afisa Leseni wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), akifuatiwa na Katibu wa Jumuiya ya Wazee Bw.Samwel Nyiru na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Deoglas Msangi. |
|
Wazee wa Jumuia ya Wazee wa Halmashauri ya Wilaya ya Same (JUWASA), wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya uzinduzin rasmi wa jumuiya hiyo, wakati wa Mkutano Mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Jimbo Katoliki, Same. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Rosemary Sitaki Senyamule, kushoto kwake ni Katibu tawala wa Same (DAS) Sospeter Magonera. Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ni mmoja wa wadhamini wa Mkutano Mkuu wa Jumuia hiyo. |
SAME.
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA imetoa elimu juu ya namna ya kusajili majina ya biashara na upatikanaji wa Leseni kwa njia ya mtandao kwa Jumuiya ya Wazee wa Wilaya ya Same (SUWASA).
Afisa msajili kutoka Wakala wa Usajili wa biashara na Leseni (BRELA), Bw. Salehe Yahaya aliwaelimisha wazee katika jumuiya hiyo juu ya huduma zinazotolewa na BRELA sambamba na kuwaeleza umuhimu wa kusajili majina ya biashara zao na kupata lesseni za biashara kundi A.
“BRELA inatoa huduma mbalimbali zikiwemo usajili wa majina ya biashara, usajili wa alama za biashara na huduma, usajili wa makampuni, kutoa hataza kwa maana ya hati miliki kwa vumbuzi ambazo zinasaidia kutatua changamoto katika jamii”
Sambamba huduma hizo pia wakala inatoa leseni kundi A ambayo itawawezesha kufanya biashara mahali popote ndani nan je ya nchi pamoja na utoaji wa leseni za viwanda. Aidha wazee hao walielimishwa kuhusu umuhimu wa kufanya sajili za biashara zao ikiwa ni pamoja na kuipa utu wa kisheria biashara zao.
Mkutano mkuu wa jumuia hiyo ya Wazee wa Halmashauri ya Wilaya ya Same ulienda sambamba na kuzindua jumuia hiyo ambayo ilizinduliwa rasmi na Katibu tawala wa Wilaya hiyo Mhe.Sospeter Magonera, BRELA ni mmoja wa wadhamini wa mkutano huo.