Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongo akimpatia zawadi ya Kitenge cha CCM Bablozi wa China Wang Ke baada ya Mazungumzo. |
Katibu Mkuu wa CCM Chongolo akimuonyesha Wang Ke picha za viongozi wastaafu wa CCM. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme. |
Balozi Wang Ke alipokuwa kwenye mazungumzo |
Katibu Mkuu wa CCM Chongo akiwa kwenye mazungumzo hayo. Pamoja naye ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Moudlin Cyrus Castico na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Dk. Hawasi Haule. |
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka wakiwa kwenye mazungumzo hayo. |
Na: Bashiru Nkoromo, DODOMA.
Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, amesema China na Mataifa mengine yanafurahishwa na mwenendo mzuri wa uongozi wa awamu ya sita chini ya Rais na Mwenyekiti wa CCM Samia Suluhu Hassan na wanatarajia Tanzania kuendelea kupiga hatua zaidi.
Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM Said Nguya, imesema Balozi Ke, amesema hayo wakati akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo alipofika Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, kuwaaga wana CCM na Watanzania kwa jumla kufuatia kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
“Tunafuraha kuona kwamba, uongozi mpya ndani ya Chama na Serikali chini ya Rais Samia unaendelea vema na uongozi umendelea kuwa imara na wenye tija kwa wananchi wake.
“Uongozi unaendelea kupata ushirikiano mkubwa sio tu ndani ya nchi bali na nje ya Tanzania, hivyo tunaamini Tanzania itaendelea kupiga hatua zaidi za kimaendeleo.” amesema Balozi Ke.
Balozi huyo, kwa niaba ya Serikali na Watu wa China amemhakikishia Katibu Mkuu kuwa, wataendelea kutoa ushirikiano wote kwa upande wa Serikali na Chama hasa kutokana na historia nzuri iliyopo kati ya CCM na Chama Cha Kikomunisti cha China CPC.
Ameipongeza CCM kwa kuvuka salama, kwa amani na utulivu mkubwa katika kipindi kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dk. John Magufuli, na kufanikiwa kumpata Mwenyekiti mpya na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Chongolo kwa niaba ya CCM amemuomba Balozi Wang Ke, kuendelea kuwa Balozi mzuri wa Tanzania nchini China kwa kuwa yeye amepata bahati ya kuishi hapa na kujionea mwenyewe utulivu na amani iliyopo.
Amemuhakikishia Balozi kuwa, ushirikiano kati ya Tanzania na China, na kati ya CCM na CPC sio wa kutiliwa shaka, ni uhusiano wa kindugu na umejengwa katika misingi ya kihistoria na kamwe hauwezi kutetereshwa.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakiwemo Naibu Katibu Mkuu Bara Christina Mndeme na Katibu wa NEC, Itkadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.
Wengine ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni Moudlin Cyrus Castico, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Dk. Hawasi Haule na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania UWT Queen Mlozi.
Credit – Blog ya Taifa ya CCM.