Waziri wa fedha na mipango Dkt Mwigulu Nchemba amezitaka Taasisi za fedha zenye sifa stahiki ikiwemo CRDB kufungua matawi nchi jirani ili kuweza kutanua wigo wa biashara na kupata faida kubwa zaidi.
Dkt Mwigulu aliyasema hayo wakati akifungua semina ya wanahisa wa banki ya CRDB iliyofanyika mkoani Arusha ambapo ambapo alisema kuwa lazima mabenki yawaze kufungua matawi kwenye nchi nyingine hasa CRDB ambayo ni Benki kiongozi.
“CRDB natambua mna tawi Burundi lakini wekezeni na kwenye nchi zingine kwani kama nchi tumechelewa sana kuwa na uwekezaji huko na hii ni kwasababu tumeridhika na sifa za kisiasa kuwa sisi ndio tuliowakomboa,” Alisema Dkt Mwigulu.
Alisema kuwa Tanzania wana uwezo wa kuongea na nchi nyingine na wakapata eneo la kufanya biashara hivyo Benki zetu AMBAZO zina sifa zikafungue matawi huko na hilo litasaidia kukuza uchumi pamoja na kutengeneza ajira.
“CRDB ni Benki kiongozi na na wana uwezo wa kuyafanya haya na sisi kama serikali tutandaa sera nzuri zitakazowasaidia kufanya biashara lakini pia kuwahudumia wananchi na tunatambua mchango mkubwa wa bank ya CRDB kwa ustawi na ukuaji wa uchumi wa Taifa la Tanzania,” Alieleza.
Alifafanua kuwa akiwa waziri wafedha anawaahidi sera nzuri za kifedha katika kufanikiwa kwa taasisi za fedha ambapo amepanga kufanya mazungumzo na taasisi za kifedha ili kuangalia ni wapi wanapo kwama na kutatua changamoto hizo ili taasisi zinazo endelea kufanya vizuri ziwe taa kwa taifa letu huko nje ya Nchi na kuweza kupata wawekezaji wengi ambao wataweza kuwekeza hapa nchini.
Aidha kwa suala la la riba Dkt Mwigulu alisema kuwa bado riba ni kubwa kwa wananchi hivyo katika mazungumzo yake na taasisi za kifedha watangalia namna ya mazingira rafiki katika kurekebisha hilo katika maeneo ambayo ni vikwazo kwenye mzunguko wa fedha ili kutoa unafuu kwa wananchi kwa ajili ya ustawi wa taifa.
kwa upande wake Naibu Gavana wa Banki Kuu ya Tanzania Dkt Bernad Kibese alieleza kuwa anaamini jitihada za kukuza ukuaji wa fedha kwenye taasisi za kifedha kwani wataweza kuongeza watanzania wenye kutambua ukuaji wa fedha ili kukuza uchumi wa Taifa.
“Naami jitihada za kukuza ukuaji wa fedha na tutaweza kuongeza watanzania wenye kutambua ukuaji wa fedha na kukuza uchumi wetu wa tanzania, CRDB imefanya jambo jema kuwaweka pamoja wanahisa kwa kuwapa elimu na kiukweli banki hii ni bank kiongozi na wa wanahisa wenu ndiyo wamiliki na mmeweza kufaidi mazuri ya uwekezaji”. Dkt Kibesa.
“Pia niwaombe mnapoendelea kutoa huduma niwaombe kiwaangalia wananchi ambao ni wengi niwaombe mzidi kuwaangalia maana wanalia sana riba za mikopo nikubwa mmno niwaombe kutoa huduma nzuri kwa wananchi kukuza ili kukuza uchumi”. aliongeza Dkt Kibesa.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB, Ally Laay alisema kuwa bado kuna ufinyo wa muamko katika swala la hisa na uwekezaji maana wananchi wengi hawaamini katika soko la hisa ambapo wakiangalia katika soko la hisa la Dar es salaam watagundua kuwa wastani wa hisa Milioni Moja na laki saba humunuliwa na kuuzwa kwa siku kwa thamani ya shilingi Milioni mia nne na sitini pekee ambapo takwimu zinaonyesha ni sawa na watanzania laki saba kati ya watanzania milioni hamsini na tatu ambayo ni sawa na asilimia 1.25.
Sambamba na hayo pia kaimu Meneja wa Kampuni Tanzu ya Bima ya Benki ya CRDB Wilson Mnzava alisema kuwa wamefanikiwa kutoa gawio la zaidi ya bilioni 1.26 kwa mwekezaji wao ambapo kampuni hiyo imesema ni mafanikio makubwa ukilinganisha na mwaka Jana ambapo waliweza kumpa gawio la sh. Milioni 500.
“Mwaka Jana tulifanikiwa kugawa gawio la sh. Milioni 500 lakini jambo lakushukuru Mungu zaidi mwaka huu tumepiga hatua kubwa na kugawa sh. Bilion 1.26 kwa mwekezaji wetu CRDB, hii ni kutokana na kupata faida kubwa kutoka kwa wateja wetu” alisema Mnzava.
Alisema kampuni ya Bima iliweza kupata faida kubwa kutoka sh. bilioni 1 hadi kufikia sh. bilioni 3.6 baada ya Kulipa kodi pamoja na gawio kwa Mwekezaji wake, huku akidai kuwa ni Mafanikio ya kiwango cha kuridhisha.
“Pamoja na kuwepo kwa janga la Corona kwa mwaka Jana sisi tumeweza kupanda na kupata faida kubwa, jambo ambalo kwetu tuliona ni maendeleo mazuri lakini pia kutokana na kampuni nyingi na mashirika kuyumba tunamshukuru Mungu hatukushuka kimapato ,tuliebdelea kuwahudumia wateja wetu kwa kiwango kilichostahili” alisema .
Alisema Kampuni Tanzu ya Bima inawalipia wateja wake gharama za Bima ya mkono wa pole kwa Mwanachama aliyefariki au kufiwa na mwenzi wake ambayo ni sh. 2,000,000 kwa akaunti za kawaida lakini kwa wenye akaunti kubwa kidogo hulipiwa milioni 5.