Home LOCAL WAFAMASIA DAWA ZOTE ZITOLEWE KWA CHETI

WAFAMASIA DAWA ZOTE ZITOLEWE KWA CHETI


DAR ES SALAAM

Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt Dorothy Gwajima, amewaelekeza wanataaluma wa kada ya famasi nchini kuhakikisha dawa zote zinatolewa kwa cheti cha dawa.

Dkt.Gwajima ameyasema hao jana  jijini Dar es Salama wakati wa mkutano  Mkuu wa mwaka wa wataalam wa famasi nchini.

Akimuelekeza mfamasia Mkuu wa Serikali katika mkutano huo, Dkt Gwajima amesema cheti cha dawa yaani (prescrition) ziwe za viwango na ziwekwe kwenye tovuti ya wizara ya Afya ili kila kituo cha kutolea huduma za afya kiwe na uwezo wa kuchapisha na sio kujitetea kuwa hazipo bohari kuu ya dawa.

Sambamba na hilo, Dkt Gwajima amewakumbusha watalaamu wa afya nchini kuzingatia maadili na miiko ya taaluma katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia taratibu za serikali katika menejimenti ya bidhaa za afya, ambapo tayari hatua kali zimeanza kuchukuliwa dhidi ya wale wanaokiuka sheria na kanuni na kuisababishia serikali hasara.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi, amesisitiza umuhimu wa nidhamu, uwajibikaji na uadilifu katika taaluma hiyo na kuwataka kupitia taaluma yao kulinda wananchi na kuacha utaratibu wa uuzaji dawa kiholela.

Naye Prof.Omari Minzi, Mwenyekiti, Baraza la Wadhamini wa Chama (PST) amesema changamoto ya udokozi wa dawa inachafua taaluma hiyo na kuwataka waache tabia hiyo kwani wengine wanakua mbuzi wa kafara hivyo amemtaka Waziri wa Afya awamulike

Mkutano huo wa wanataaluma wa kada ya famasi umebeba kauli mbiu isemayo wataalamu wa famasi; ni muhimu katika kuboresha upatikanaji wa dawa bora Tanzania, kauli mbiu ambayo inatekelezwa na serikali katika kuhakikisha dawa zinapatikana kupitia bajeti ya dawa ambayo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, kwa mwaka huu wa fedha serikali imeshatoa shilingi bilioni 121.3 zikiwemo bilioni 80 zilizotolewa mwezi April 2021.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here