Home BUSINESS TWCC YAMPONGEZA MHE. RAIS SAMIA KUONGEZA FURSA ZA KIBIASHARA NA KENYA.

TWCC YAMPONGEZA MHE. RAIS SAMIA KUONGEZA FURSA ZA KIBIASHARA NA KENYA.

Mwenyekiti wa TWCC Taifa Bi. Mercy Silla Akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) Katika mkutano wao maalum wa Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ofisini  kwao Jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Bodi ya TWCC wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama hicho Bi. Mercy Silla wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Mei 6 Jijini Dar es Salaam.

Na: Hughes Dugilo DAR ES SALAAM.

Chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania TWCC kimesema kuwa ziara aliyoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan nchini Kenya imeleta matumaini mapya katika kuboresha uhusiano wa nchi hizo mbili hususan kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao bila vikwazo vyovyote.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Mei 6 katika Ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaa Mwnyekiti wa TWCC Taifa Bi. Mercy Silla amesema kuwa ziara hiyo imefungua milango ya kibiashara nakwamba wao wanajipanga kimkakati kuhakikisha wanachama wao wanakuwa mstari wa mbele kwa kuongeza uzalishashaji wa bidhaa zao.

Akizungumzia hotuba ya Mhe. Rais Samia, Bi. Silla amesema kuwa katika Jumuiya ya Mashariki Tanzania ina mipaka mingi na kenya na kwamba asilimia 75 ya biashara za mipakani zinafanywa  na wanawake hivyo wanaamini wataendelea kufanya biashara ndogo ndogo ikiwemo kuuza mazao nchini kenya ambako kunategemewa kwa soko.

“Kenya ni nchi ambayo tunafanyanayo biashara kwa ukaribu sana na tunafahamu kihistoria kabisa kwamba miaka mingi tunafanya biashara na kenya na hasa kwenye mipaka, na kule kwenye mipaka ukiangalia wanawake ndio wengi kwahiyo sisi tunaamini kwa mawasiliano na mahusiano ambayo yameanza kujengwa tena na Rais wetu hiyo inatupa moyo sisi wakinamama hasa wale wanaofanya biashara kule kwenye mipaka na tunafahamu kwamba biashara nyingi zinafanyika kule mipani” amesema Mercy Silla

Aidha ameongeza kuwa wao kama wanawakake wafanyabiashara wataendelea kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Samia katika kuinua uchumi wa mtanzania kwa kufanya kwa kushikiriki katika shughuli za maendeleo na kwamba wanaamini kuwa kwa kufanya hivyo italeta ustawi wa pamoja katika kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

“Tunashukuru sana kwakweli na kwa kuwa Mama amesema kazi iendelee na inaendelea na sisi wanawake wafanyabiashra tutaendelea kushiriki katika ujenzi wa uchumi na maendeleo ya nchi yetu” Ameongeza.



LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here