Home SPORTS SIMBA YAWAPA HAMASA WACHEZAJI WAO KUIUA KAIZER CHIEFS DIMBA LA MKAPA J.MOSI.

SIMBA YAWAPA HAMASA WACHEZAJI WAO KUIUA KAIZER CHIEFS DIMBA LA MKAPA J.MOSI.

Afisa Habari wa Simba SC, Hajji Sunday Manara akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo hoteli ya Serena, Dar es Salaam. 

Na: Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Simba SC umewatak wachezaji wake kujituma kwa zaidi ya asilimia 100 ili kuitoa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hayo yamesema na Afisa Habari wa Simba SC, Hajji Sunday Manara kuekelea mchezo wa marudiano Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

“Kama tunahitaji kushinda jumamosi lazima wachezaji wetu wajitoe kwa asilimia 100, wanaweza wakiamua. Tunawaamini mnaweza kupindua matokeo na kuleta heshima Msimbazi. Wanasimba wanataka kufuzu, hatutaki kujitahidi, Simba sio timu ya kujitahidi, ni timu ya kufuzu,”amesema Manara katika mkutano na Waandishi wa Habari mchana wa leo hoteli ya Serena, Dar es Salaam.

Manara amesema mashabiki wanaiamini timu yao inaweza na wao uongozi wamejiandaa kikamilifu na mchezo wa Jumamosi wakiamini wachezaji watapokea maelekezo vizuri kutoka kwa walimu na kushinda.

Ameongeza kwamba kaulimbiu ya Simba kuelekea mchezo huo ni “Ama Zetu Ama Zao; Do or die season 2,” na kuhusu mashabiki Manara amesema Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeruhusu watu wasiozidi 10,000 kuingia uwanjani, ingawa wao wanaendelea kuomba waongezewe idadi.

Amemtaja Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, mwana SImba mzuri, Amos Makala kuwa mgeni rasmi siku hiyo.

“Tunawapa sana heshima Kaizer Chiefs, ni timu nzuri lakini tunao uwezo wa kupindua matokeo. Simba ikishinda mechi hii nchi itapata heshima, lakini pia tutakuwa tumeandika rekodi,”ameongeza.

Simba inatakiwa kushinda 5-0 ili kwenda Nusu Fainali kwa mara ya kwanza tangu 1974 baada ya kuchapwa 4-0 Jumamosi kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi wa Uwanja wa FNB, Johannesburg – jambo kocha kocha Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa amesema linawezekana.

Credit- Bin Zubeiry Blog.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here