Home LOCAL MAKABIDHIANO YA OFISI KATI YA RC KUNENGE NA RC MAKALA YAFANYIKA.

MAKABIDHIANO YA OFISI KATI YA RC KUNENGE NA RC MAKALA YAFANYIKA.

DAR ES SALAAM.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambae kwa Sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge leo May 19 amekabidhi ofisi kwa Mkuu Mpya wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makala ambapo amewashukuru Watumishi wote wa Mkoa huo kwa ushirikiano mkubwa waliompatia wakati wa uongozi wake.

RC Kunenge amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Imani kubwa aliyomuonyesha kwa kumteua kuongoza Mkoa wa Pwani.

Aidha RC Kunenge amesema ushirikiano wa kazi baina yake na Watumishi wote wa Mkoa viliwezesha kupatikana kwa mafanikio makubwa ambapo ametoa wito kwa Watumishi hao kuendelea kumpa ushirikiano huohuo Mkuu wa Mkoa Mpya ili aweze kutimiza maono ya Rais Samia Katika Mkoa huo.

Kwa upande wake Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makala amempongeza RC Kunenge kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya Katika Mkoa huo na kueleza kuwa anaamini uwezo alioonyesha Dar es salaam ataupeleka Mkoa wa Pwani.

Makabidhiano ya ofisi yamefanyika mbele ya Viongozi wa Mkoa huo akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wastaki Meya, Viongozi wa Usalama, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakuu wa Idara.

Previous articleSIMBA YAWAPA HAMASA WACHEZAJI WAO KUIUA KAIZER CHIEFS DIMBA LA MKAPA J.MOSI.
Next articleKARIBU USOME HABARI MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 20-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here