Home LOCAL SHULE YA BILIONEA LAIZER YAKABILIWA NA UHABA WA WALIMU.

SHULE YA BILIONEA LAIZER YAKABILIWA NA UHABA WA WALIMU.

Mwalimu mkuu wa shule ya kingereza ya Saniniu Lizer Swedefrida Msoma
Hawa ni baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo

Na:Richard Mrusha, MANYARA.

Bilionea Saniniu Lizer amewomba wadau wa sekta ya Madini Mkoa wa manyara kumuunga mkono katika jitahada za kuendeleza Ujenzi wa shule ya kingereza ya Saniniu Lizer iliyopo  wiliya ya simanjiro kata ya Naisinyai   Kijiji Cha Naepo.

Lizer amesema kuwa wachimbaji wadogo wadogo waliopo manyara wakati umefika wa kuonana umuhimu wa kuleta maendeleo katika mkoa wao Kwani 

wanapata pesa kutokana na uchimbaji wa Madini yaliyopo mkoani hapo hivyo waguswe kusaidia Jamii ya kimasai kwani wamasai wakipewa elimu itawesadia sana.

Hayo ameyasema leo wakati akiongea na waandishi wa habari walioenda kujionea shule hiyo aliyoijenga na Kisha kuikabidhi kwa serikali January 13 mwaka 2021

Amesema  kuwa muitikio ni mkubwa kwani mpaka Sasa watoto walioandikishwa  shuleni hapo ni miambili tisini na tatu (293) na wanafurahia kwa kupata huduma ya  shule ya kingereza jirani na makazi yao tofauti na uko nyuma walikuwa wakienda mbali kupata huduma ya elimu,”amesema Lizer.

Ameongeza kuwa kwa kuwepo kwa shule hiyo kumeweza kufungua wigo Hadi kwa watu wazima wa Jamii ya KI Masai ambapo tumetengea mda wa masaa matatu kwa ajili ya kuja kupata elimu hawa ni watu ambao walikosa elimu uko nyuma nao Sasa wanaokuja hap kupata elimu.

Ameongeza kuwa Sasa wanataka kujenga bwalo la kulia chakula na wako kwenye maandalizi na Sasa wameishaleta tofari kwa ajili ya Ujenzi uho na pia watajega mabweni kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka mbali ili waweze kukaa hapa.

Kuhusu changamoto Lizer amesema anaiomba serikali ya awamu ya 6 Inayoongozwa na Rais Samiha Suluhu Hassani kuweza kuwaongezea walimu hapo shule kwani  mpaka Sasa Ina waalimu wawili (2) tu ambao wanafundisha watoto miambili na tisini na tatu (293) na pia serikali iweze kuwasaidia katika Ujenzi wa mabweni.

Ameongeza kuwa kuwa nilijenga hii shule kwa lengo la kuwasadia watoto wa Jamii ya kimasai ili wasome na sio kwamba Nina hela nyingi kiasi kwamba siitaji tena hela hapana! Lengo langu au, kiu yangu nikuona Jamii ya kimasai inapata elimu ili badae nao waje kusaidia Jamii yetu.

kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Swedefrida Msoma amesema mpaka Sasa muitikio ni mkubwa Sana na wameweza kuandikisha zaidi ya wanafunzi miambili na tisini na tatu (293)  amesema Jamii ya kimasai ni watu ambao wana akili sana maana watoto waliopo hapa shuleni tumewafundisha kwa mda mfupi na wameweza Kuelewa.

Amesema  Kuwa mwanzoni kulikuwa na ugumu kwasababu ya mawasiliano kwa maana ya lugha kwakuwa walizoea kuongea kugha ya kimasai tu Ila kwasa wanaweza kuongea lugha ya kiswahili na kingereza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here