Home LOCAL SHILINGI MILIONI 250 KUKAMILISHA MABOMA MATANO YA ZAHANATI SINGIDA

SHILINGI MILIONI 250 KUKAMILISHA MABOMA MATANO YA ZAHANATI SINGIDA

Na: Maiko Luoga

Serikali imepanga kutumia Shilingi milioni 250 katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya kukamilisha maboma matano ya Zahanati katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida Mkoani Singida ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wananchi katika kujenga na kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt.Festo Dugange wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Mheshimiwa Abeid Ighondo Ramadhani aliyetaka kujua ni lini Serikali itamaliza ujenzi wa maboma ya Vituo vya Afya yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi katika Kata za Makuro na Ngimu.

Dkt. Dugange amesema katika mwaka wa fedha 2020/2021 Serikali ilitenga Shilingi milioni 150 kwa ajili ya kukamilisha maboma ya Zahanati za Minyeye, Mnung’una na Msikii katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Aidha Naibu Waziri amesema kuwa ili kuboresha huduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida katika mwaka wa fedha 2018/19 Serikali iliipatia Halmashauri hiyo Shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri.

Pia Katika mwaka wa fedha 2020/21 Hospitali hiyo ilitengewa Shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wa wodi tatu na Shilingi milioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.

Previous articleVIJANA 2,563 WAPATIWA MAFUNZO YA KILIMO HAI DODOMA
Next articleMAZAO YA KILIMO HAI YANA UHAKIKA WA SOKO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here