Home LOCAL SERIKALI KUZINDUA MFUMO WA KIELEKTRONIKI KUDHIBITI UHAMISHO WA WATUMISHI.

SERIKALI KUZINDUA MFUMO WA KIELEKTRONIKI KUDHIBITI UHAMISHO WA WATUMISHI.

 Na:Maiko Luoga.

Serikali imeandaa mfumo wa kielektroniki  ili kuchuja kwa uhakika uhamisho wote unaoombwa na kuwezesha Watumishi wa maeneo ya Vijijini kubaki katika maeneo hayo wakiendelea na majukumu yao badala ya kuomba kuhamia maeneo ya mijini.

Hayo yamesemwa mei 06/2021 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt, Festo Dugange wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Mkoani Tanga Mhe, Timotheo Mnzava aliyetaka kujua utaratibu wa Serikali juu ya kuwadhibiti Watumishi wanao ajiriwa Vijijini kisha baada ya muda mfupi kuomba kuhamia Mijini.  

“Ofisi ya Rais TAMISEMI na Serikali kwa ujumla imeendelea kuhakikisha inazingatia ikama ya Watumishi katika maeneo ya Vijijini na imeendelea kuhakikisha inasimamia kwa karibu uhamisho wa Watumishi hasa kutoka Vijijini kwenda mijini, Tumekuwa tukichuja sababu za msingi ambazo zinapelekea baadhi ya Watumishi kukubaliwa na wengine kuto kukubaliwa kupata uhamisho, Dkt, Festo Dugange.

“Ili kudhibiti hili Serikali imeweka utaratibu Ofisi ya Rais TAMISEMI tunaenda kuzidua mfumo wa kielektroniki ambao maombi ya uhamisho wote yatapitishwa kwa mfumo huo na kuwezesha kuchuja kwa uhakika hamisho zote zinazoombwa na kuwezesha Watumishi kubaki katika maeneo ya Vijijini kufanya kazi walizopangiwa” alieleza Dkt, Festo Dugange Naibu Waziri Ofisi TAMISEMI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here