Home LOCAL RC MAKALLA AAGIZA JESHI LA POLISI KUTOKOMEZA UJAMBAZI DAR, AWATAKA WAHALIFU KUJISALIMISHA...

RC MAKALLA AAGIZA JESHI LA POLISI KUTOKOMEZA UJAMBAZI DAR, AWATAKA WAHALIFU KUJISALIMISHA NA SILAHA ZAO MARA MOJA.


DAR ES SALAAM.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuhakikisha linawashughulikia kikamilifu Majambazi na Vibaka Jijini humo huku akiwataka kujisalimisha na kukabidhi Silaha zao kwa hiyari.

RC Makalla ameagiza kuanza kwa Operesheni ya kufagia watu wote wanaofanya Vitendo vya uhalifu Jijini humo ambapo amesema ni vyema pia Wazazi wakaanza kuwaonya watoto wao pindi wanapoona Wana mienendo isiyoeleweka.

Aidha RC Makalla amesema kwakuwa uzoefu unaonyesha wahalifu hao hutumia Silaha kujerui na kusababisha vifo, ni vyema Jeshi la Polisi likawawahi kuwashughulikia kikamilifu Majambazi kabla hawajatumia Silaha hizo kujerui na kusababisha vifo kwa Wananchi.

Hata hivyo RC Makalla amewahikikishia Wananchi Usalama na kuwataka kuendelea na majukumu yao Kama kawaida kwakuwa Vyombo vya usalama vimejidhatiti kulinda usalama wao na mali zao.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Camilius Wambura amesema Katika msako ulioanza May 21 adi May 25 wamefanikiwa kuwakamata Majambazi na Vitu mbalimbali ikiwemo magari Manne, Pikipiki moja, Bunduki Moja, Laptop na vifaa vinginevyo.

Aidha Kamanda Wambura amemuhakikishia RC Makalla kuwa maagizo aliyoyatoa wameyapokea kwa mikono miwili na watayafanyia kazi kwa ufanisi mkubwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here