Home LOCAL RC KUNENGE AFUTURISHA MAKUNDI MBALIMBALI YA WANANCHI DAR, MUFTI WA TANZANIA ATOA...

RC KUNENGE AFUTURISHA MAKUNDI MBALIMBALI YA WANANCHI DAR, MUFTI WA TANZANIA ATOA NENO.

DAR ES SALAAM.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakar Kunenge leo May 10 amefuturisha Makundi Mbalimbali ya Wananchi wakiwemo Walemavu wa Viungo, Wasioona, Wasiosikia, Wenye ulemavu wa Ngozi, Wajane, Wasiojiweza, Yatima na Wadau wa maendeleo ambapo Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Ally ametumia hafla hiyo kutangaza utaratibu wa Sala ya Eid kitaifa na Baraza la Eid.

Mufti wa Tanzania amesema Sala ya Eidk itasaliwa Viwanja vya Mnazi Mmoja na Baraza la Eid litafanyika Ukumbi wa Karimjee ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa  kuwa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi.

Aidha Mhe. Mufti amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakar Kunenge kwa kuona umuhimu wa kufutarisha Wananchi wa Makundi mbalimbali Jijini humo ambapo amesema kitendo hicho ni sadaka njema mbele za Mungu.

Akizungumza Katika hafla hiyo, RC Kunenge amewashukuru Wananchi walioitika wito wake kwa kujitokeza kwa wingi kuungana nae Katika futari huku akitoa shukrani za dhati pia kwa Wadau walioshirikiana nae kufanikisha Jambo hilo.

Tukio la Iftar ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ilifanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee na kushirikisha mamia ya wananchi wa Dar es salaam.
Previous articleMAGAZETI YA LEO J.NNE MEI 11-2021
Next articleMEYA KUMBILAMOTO AWAPONGEZA JIJI KWA HATI SAFI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here