Home LOCAL RAMANI ZA UJENZI SASA KUPELEKWA ZIMAMOTO.

RAMANI ZA UJENZI SASA KUPELEKWA ZIMAMOTO.

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo(Kushoto), akiukagua msokoto wa bangi wakati alipotembelea Banda la Jeshi la Polisi wakati  wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto ambapo alipata maelezo mbalimbali kuhusu madawa ya kulevya  na jinsi jeshi la polisi linavyodhibiti uhalifu unaohusiana na dawa za kulevya nchini.Maadhimisho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo(katikati), akisikiliza maelezo ya jinsi ya kupambana na moto katika majengo ya ghorofa wakati alipotembelea banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yanayofanyika katika Viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro.Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo,John Masunga.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionyesha jinsi ya kumuokoa mhanga wa ajali ya barabarani wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto, iliyofanyika katika Viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionyesha jinsi ya kumuingiza katika gari ya dharura ya  wagonjwa mmoja wa majeruhi wa ajali ya barabarani wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto, iliyofanyika katika Viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo(kulia), akionyeshwa jinsi ya kusoma alama za uhalifu katika eneo la tukio wakati  wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto ambapo alipata maelezo mbalimbali jinsi jeshi la polisi linavyochukua alama za upelelezi wa kimazingira.Maadhimisho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Na: Mwandishi Wetu, MOROGORO..

Serikali imewashauri wananchi kupeleka ramani zao za ujenzi kwa wataalamu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili waweze kupata ushauri wa kitaalamu katika miradi yao ya ujenzi lengo ikiwa ni kuepusha madhara pindi yanapotokea majanga ya moto.

Ushauri huo umetolewa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya zimamoto katika Viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro

“Askari wetu wa Zimamoto wamekua wakipata shida kuyafikia maeneo na majengo mbalimbali pindi yanapotokea majanga mbalimbali ikiwemo moto,hali inayopelekea kuteketea kwa mali nz thamani mbalimbali,sasa natoa rai kwa wananchi kuwasiliana na wataalamu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili waweze kupata ushauri wa kitaalamu kupitia ramani zao za ujenzi “ alisema Chilo

Sambamba na ushauri huo pia Naibu Waziri huyo amewaomba wananchi kuwaunga mkono Jeshi la Zimamoto kwani kazi wanazofanya zinahitaji ujasiri mkubwa nani kazi za hatari huku akiwaasa kuchukua tahadhari za usalama dhidi ya majanga ya moto na mengineyo.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,John Masunga alielezea dhana ya maadhimisho hayo kuwa ni kuenzi wahanga wote waliopoteza Maisha katika ajali za moto na kuwaezi kwa namna walivyojitoa katika kuokoa Maisha na mali za watu wengine huku wakihatarisha Maisha yao.

“Ni siku muhimu ikiwa tunawakumbuka wapendwa wetu basi tuchukue tahadhari kwa vyanzo mbalimbali vinavyosababisha majanga ya moto na yanayofanana na hayo na sisi jeshi la zimamoto tunajitahidi kutoa elimu mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wetu waelevu katika kuhakikisha maisha ya wananchi na mali zao zinakua salama” alisema Kamishna Jenerali John Masunga.

Katika maadhimisho hayo maonesho mbalimbali yalionyeshwa yakihusiana na kinga na tahadhari sambamba na elimu ya maokozi ambapo wanafunzi kutoka shule za mkoani Morogoro kupitia Chama cha Skauti Tanzania walipata mafunzo hayo pia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here