Home LOCAL RAIS SAMIA KUTARAJIWA KUWA MGENI RASMI BARAZA LA IDDI MWAKA HUU.

RAIS SAMIA KUTARAJIWA KUWA MGENI RASMI BARAZA LA IDDI MWAKA HUU.

Na: MWANDISHI WETU.

Baraza la Waislam nchini  Bakwata, limetangaza kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Iddi mwaka huu, atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Samia Hassani Suluhu.

Baraza hilo litafanyika katika ukumbi wa Karimjee, baada ya swala ya Iddi ambayo kitaifa itafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na waandishi wa habari Sheik Mkuu mkoa wa Dar es Salaam Alihad Mussa Salum, katika Iftari iliyo andaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Abubakai Kunenge, amewataka waumini wa dini zote kujitokeza kwa wingi katika baraza la Iddi ili kuja kumsikiliza kiongozi wetu wa nchi.

“Mwaka huu tumepata bahati katika baraza la Iddi mgeni rasmi atakuwa rais wetu tayari amethibitisha uwepo wake, niwaombe waumini na wasio waumini wa kiisila kujitokeza kwa wingi ili kumshukuru Mungu na kupokea nasaha za kiongozi wetu,” anasema 

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Abubakari  Kunenge amewashuku wote waliojitokeza katika Iftari hiyo ambayo ili lenga watu kutoka katika makundi tofauti katika mkoa wake.

“Nipende kuwashukuru mliofika hapa nimeenda Iftari hii kwa ajili ya kukutana na wawakilishi wa makundi ya watu mbalimbali ikiwemo wenye uhitaji, kwa kuwa imani yangu inanitaka kufanya hivyo,” anasema Kunenge.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here