Home LOCAL RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA KIWANDA CHA USHONAJI CHA JESHI LA...

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA KIWANDA CHA USHONAJI CHA JESHI LA POLISI TANZANIA -KURASINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akivuta utepe kufungua Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam leo tarehe 18 Mei, 2021. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Khamis Hamza Khamis pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro mara baada ya kufungua Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam leo tarehe 18 Mei, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipiga makofi na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Khamis Hamza Khamis pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi wa Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam leo tarehe 18 Mei, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua kazi mbalimbali zinazofanywa katika kiwanda hicho cha ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam mara baada ya kukifungua leo tarehe 18 Mei, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua kazi za upimaji na ukataji wa vitambaa vinavyotumika katika kushona sare za Jeshi la Polisi katika Kiwanda cha Ushonaji Nguo cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Polisi Kurasini mkoani Dar es Salaam mara baada ya kufungua Kiwanda hicho cha Ushonaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Askari pamoja na Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi pamoja na Wageni wengine Kurasini mkoani Dar es Salaam mara baada ya kufungua Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania.

PICHA NA IKULU.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here