Home LOCAL OFISI YA MBUNGE KAMONGA YAANZISHA KAMPENI YA UCHUMI LUDEWA.

OFISI YA MBUNGE KAMONGA YAANZISHA KAMPENI YA UCHUMI LUDEWA.

Mbunge Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga.

Mtaalamu wa Uchumi Lucia Mwaipopo akizungumza wakati wa kutoa Elimu kwa wananchi na wajasiriamali wa Wilaya ya Ludewa juu ya fursa hiyo muhimu iliyoletwa na Mbunge wao.

Na: Damian Kunambi: NJOMBE.

Ofisi ya mbunge jimbo la Ludewa Joseph Kamonga imeanzisha programu ya kutoa elimu kwa wananchi  wilayani Ludewa iliyopewa jina la KAMPENI YA UCHUMI iliyolenga kuwaelimisha wananchi hao kutambua fursa zilizopo kata kata zao na wilaya kwa ujumla pamoja njia ya kuzitumia fursa hizo ambayo tayari yameanzakwa baadhi ya kata na yanatarajiwa kuwafikia wananchi katika kata zote 26 za wilaya hiyo.

Program hiyo ambayo itafanyika kwa awamu kwa kipindi cha miaka miwili yamelenga kuelimisha jamii na vikundi mbalimbali ili kuweza kuzitumia fursa hizo kama fursa za kilimo, uvuvi na nyinginezo za kimkakati na kukuza uchumi ambapo mpaka sasa tayari wamekwishatoa elimu katka kata ya Manda, Luhuhu, Ludewa,  masasi, Mundindi,Luilo pamoja na Mavanga 

Akizungumza katika mikutano ya kutoa elimu hiyo iliyofanyika katika baadhi ya kata katibu wa mbunge huyo Alphonce Mwapinga amesema ofisi ya mbunge inatambua umuhimu wa wananchi wake katika kukua kiuchumi hivyo ikaona itoe fursa hiyo kwa wanchi ili waweze kupata elimu kwa kuwaleta mtaalamu wa uchumi ili awape darasa.

Aidha kwa upande wa mtaalam wa uchumi Lucia Mwaipopo amesema anamshukuru mbunge huyo kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo ya kutoa elimu kwa wananchi wake ambapo kwa sasa ameanza kwa kuvitambua vikundi mbalimbali na mahitaji yake pamoja na fursa zilizopo katika kata hizo.

Previous articleDC SABAYA ASIMAMISHWA KAZI.
Next articleLIVERPOOL YAICHAPA MAN U. 4-2

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here