Home LOCAL MUFTI : SIKUKUU YA EID NI IJUMAA MEI 14-2021

MUFTI : SIKUKUU YA EID NI IJUMAA MEI 14-2021

DAR ES SALAAM

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Ally amesema hakuna taarifa za kuandama kwa mwezi leo na hivyo Waislamu wataendelea kufunga na kujiandaa na Sikukuu ya Eid Ijumaa ya Mei 14, 2021, anaripoti Mwandishi Diramakini.


Sherehe za Eid El- fitr kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Dar es Salaam, swala ya Eid itaswaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 1:30 asubuhi.


Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limesema Baraza la Eid litafanyika katika viwanja vya Karimjee kuanzia saa 8:00 mchana.


Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here