Home Uncategorized MO NDASHA MJASIRIAMALI ALIEJIPANGA KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

MO NDASHA MJASIRIAMALI ALIEJIPANGA KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

 

Na: Saimon Mghendi: KAHAMA.

MAKAMPUNI pamoja na wadau wengine wenye uwezo wa kifedha wameombwa kuwasaidia makundi ya vijana katika maeneo Mbalimbali ili kuwawezesha kufikia ndoto zao.

Ombi hilo limetolewa leo na Mjasiriamali Mozes Salehe,  ambaye pia ni mmiliki wa Hoteli ya Ndasha iliyopo katika Manispaa ya Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga

Mozes Salehe ambaye pia ni maarufu kwa jina la MO NDASHA amesema kuwa ameamua kuwekeza na kuwapa fursa vijana ili kupunguza changamoto zinazo wakabili vijana wengi kwa sasa.

Mbali na kutengeneza ajira kwa vijana ambao ni zaidi ya 50 wanaofanya kazi kwenye hoteli yake pia mjasiriamali huyo anadhamini mashindano mbalimbali ya mpira wa miguu yanayoendelea katika Manispaa ya Kahama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here