DAR ES SALAAM.
Serikali kupitia wakala wa Nishati Vijijini REA imesema kuwa imeanza utekelezaji wa kupeleka umeme katika vijiji vya kata ya Ugala jimbo la Nsimbo Mkoani Katavi wenye thamani ya zaidi ya Bilioni2.46.
Hayo yamezungumzwa leo bungeni Jijini Dodoma na Naibu waziri wa Nishati Steven Biabato alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Nsimbo Anna Richard Lupembe aliyetaka kujua ni lini wananchi wa Kata ya Ugala watapatiwa umeme wa Rea awamu ya tatu?
Naibu waziri Biabato amesema kuwa kazi ya kupeleka umeme katika kata hiyo umehusisha ujenzi wa msongo wa kilovolti 33 sambamba na kufunga Transforma 3.
Katika swali lake la Nyongeza Mh. Anna Lupembe amesema kuwa hakuna dalili zozote za uwepo wa mradi wa umeme huku akimtaka naibu waziri wa Nishati kuongozana naye katika eneo la utekelezaji wa mradi huo.
Akimalizia swali lake la msingi Mh. Lupembe amehoji ni muda gani ambao wananchi wanatakiwa kufungiwa umeme baada ya muda gani baada ya wananchi kulipia gharama ambazo zinahitajika?
Akijibu maswali hayo Mh. Baibato amesema kuwa mradi huo ulizinduliwa mwezi wa Tatu na kuongeza kuwa mpaka kufikia mwezi wa 9 mwaka huu kila kijiji kitakuwa na umeme.
Akijibia kuhusu muda wa wananchi waliolipia umeme kucheleweshewa huduma hiyo Waziri wa Nishati Medad Kalemani amewataka wakandari kuripoti katika maeneo ya kazi sambamba na ofisi ya mbunge huyo ili waweze kutambulika wanapotekeleza majukumu yao.