Katibu mkuu wizara ya Ujenzi na uchukuzi Gabriel Migire akizungumza na waandishi wa habari kwenye Kakao kazi |
Mkurugenzi wa TASAC, Bwana Kaim Mkeyenge akizungumza na waandishi wa habari. |
Na: Richard Mrusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Gabriel Migire amewataka shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kuhakikisha shughuli zao wanazifanya kwa uwazi kwa kuwashirikisha wadau ili kuepusha malalamiko yanayotokea.
Agizo hilo amelitoka leo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa usafiri wa usafilishaji mizigo majini, ambapo kikao hicho kilikuwa na lengo la kujengeana uwelewa kuhusu sera.
Migire amesema kuwa TASAC imekuwa ikitekeleza majukumu yake bila kuwashirikisha baadhi ya wadau, hivyo kupelekea migogoro isiyokuwa ya lazima miongoni mwa watumiaji.
“Hivi karibuni TASAC imelalamikiwa ndani ya bunge kudai ivunje bodi kutokana utendejikazi wao kwakukuwa hauwekwi wazi kwa umma hivyo kuanzia sasa majukumu yenu mnayofanya hakikisheni yanajulikama” amesema Migire.
na kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa (TASAC ) Kaimu Mkeyenge, amesema kuwa licha ya kuwepo malalamiko yaliyokuwa yakitokea inatokana na baadhi ya wadau kutojua sera za shirika hilo.
“Kikao hichi cha leo tumejadili kanuni za usimamizi wa bandari ambayo wadau wametoa maoni yanayokwenda kufanyiwa kazi na kupatiwa ufumbuzi ili kuepusha malalamiko” amesema Mkeyenge.
na kwa upande wake Rais wa Wakala wa Forodha Tanzania Bw. Edward Urio amesema kuwa kumekuwa na mkanganyiko katika utekelezaji wa majukumu hasa katika usafilishaji wa mizigo bandarini.
Bw. Urio ameiomba Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ili kazi zinazofanyika zisilete mkanganyiko na kuepuka wateja wanaotumia bandari Tanzania kukimbia na kwenda kutumia bandari za nchi nyengine.