Home BUSINESS Kampuni ya bima ya Strategis yajitosa kuhudumia Arusha

Kampuni ya bima ya Strategis yajitosa kuhudumia Arusha

 

Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Zakaria Muyengi (kutoka kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Strategis (kitengo cha Bima za afya), Dk. Flora Minja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategis (Bima za maji na ajali), Jabir Kigoda wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa ofisi mpya ya kampuni hiyo jijini Arusha jana. kulia ni Meneja Mkuu wa Strategis, Nirmal Sheth.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategis (Bima za mali na ajali), Jabir Kigoda, akizungumza katika hafle hiyo mjini Arusha jana.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategis (kitengo cha Bima za afya), Dr. Flora Minja, akihutubia wakati wa uzinduzi huo mjini Arusha jana.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Masoko na Utafiti wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Zakaria Muyengi (katikati), akipozi kwa picha na kutoka kushoto; Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Strategis, Dennis Nombo, Ofisa Mwwndeshaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Dr. Malav Manek, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Strategis (kitengo cha Bima za afya), Dk. Flora Minja, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategis (Bima za Mali na ajali), Jabir Kigoda na Meneja wao Mkuu, Nirmal Sheth muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi.
Na Mwandishi Wetu, Arusha | KAMPUNI ya Bima ya Strategis, ikiwa ni kampuni binafsi ya bima ya pili kwa ukubwa nchini na moja ya makampuni ya mwanzo kusajiliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa shughuli za Bima Tanzania (TIRA) na ambayo imekuwa ikifanya biashara kwa zaidi ya miongo miwili, imezindua rasmi ofisi yake jijini Arusha.

Akiongea katika uzinduzi huo mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Masoko na Utafiti wa TIRA ambaye alikuwa ni mgeni rasmi, Zacharia Muyengi, alisema kuingia kwa kampuni hiyo jijini Arusha kutanufaisha wakazi wa jiji hilo na maeneo jirani na hivyo kuchangia kuongeza idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za bima kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 15.

Ni asilimia 15 tu ya Watanzania ndio wanatumiahuduma za bima, mkakati wetu ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030 asilimia 50 ya watu watakuwa wanatumia huduma hizo,, na wakati huo huop kiwango cha uelewa wa maswala ya bima kitaongezeka kutoka asilimia 30 ya sasa hadi asilimia 80,” alisema Muyengi.

Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kuwezesha makampuni ya bima kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, tunategemea watoaji wa huduma hizo nao wataitikia wito wa serikali kwa kulipa wateja wao kwa muda muafaka. Nachukua fursa hii kutoa wito kwa makampuni ya bimakuja na bidhaa zinazokizi mahitaji ya Watanzania, kama vile wavuvi, wafugaji na wakulima.

Vilevile aliipongeza kampuni ya Strategia na kuiomba kuendeleza utamaduni wakewea kulipa madai ya wateja wake kwa muda unaofaa. Alisema: “Sisi TIRA kwa upande wetu tunafurahishwa na namna kampuni ya Strategis inavyofanya kazi, wana uwezo wa kifedha wa kutosha na wanafanya malipo kwa haraka

Uzinduzi wa ofisi hii ya mauzo ni sehemu ya uamuzi wa kimkakati wa Strategis kuboresha ufanisi na manufaa ya shughuli zake katika jiji la Arusha na kanda nzima ya kaskazini.

Katika mwaka uliopita, kampuni ya Strategis iliimarisha ukuaji wake na kukua kwa asilimia 20 hadi kushika nafasi ya kampuni binafsi ya bima ya pilli kwa ukubwa nchini Tanzania kwa kuzingatia umiliki wa soko. Wakati kampuni hii inaendeela kuongoza katika bima ya afya kwa sekta ya binafsi, shughuli zake zisizo za afya zimekua kwa asilimia 40 kwa mwaka 2020. Ukuaji huu unatokana na marekebisho ya kimuundo yaliyofanywa na kampuni hiyo kuimarisha nafasi yake katika sekta ya bima, pamoja na kuungwa mkono na wadau mbalimbali.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategis (Kitengo cha Tiba) ambaye pia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni la Strategis, Dr. Flora Minja,alisema kuwa kampuni hiyo ilikuwa inatilia mkazo katika kukuza wigo wa huduma zake, kuzindua huduma mpya na kutumia teknolojia na ubunifu katika utoaji wa huduma.

Hivyo basi mkakati wetu ni kuhakikisha kuwa tunakwenda sambasamba na maendeleo ya teknolojia ambayo zinaongeza ufanisi na usahihi katika kutunza za taarifa za wateja, na tutahakikisha kuwa tunakwenda na wakatina maendeelo ya teknoloji yanayotokea kwenya sekta ya bima na kuwasiliana na wadau mbaliombali kwa muda muafaka.

Kampuni ya Strategis inaunga mkono ajenda ya huduma ya bima kwa wote, na inaunga mkono lengo la serikali na watoa huduma za bima lakuhakikisha kuwa ifikapomwaka 2030 angalau asilimia50 ya wananchi watakuwa wanatumia huduma za bima. Ili kufaniklisha hili,kampuni yetu inanui kupanua eneo lakelaklutoa huduma, na ofisi hii ya Arusha ni miongoni mwa mikakati ambayo inatarajiwa kuhakikisha kuwa tunafikia kila kikundi nchini,” Alisema Dr. Flora.

Awali akiongea katika uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Strategis (huduma zisizo za tiba), Jabir Kigoda, alisema kampuni hiyo imejizatiti kutoa huduma za kiwango cha juu kwa mkoa wa Arusha, mkakati ambao utaimarishwa na uzinduzi wa bidhaa zinazolenga sekta ya utalii, pamoja na sekta nyinginezo za uchumi kama viwanda na uzalishaji.

Uzinduzi wa ofisi yetu ya Arusha ni kiashirio cha namna gani tumejiandaa vyema kuhudumia soko labima na kunga mkono harakati za serikali za kuongeza uelewa na matumizi ya huduma za bima nchini,’ akisema Kigoda.

Aliongeza Kigoda: “Uzinduzi hu unaofanyika leo ni zaidi ya ufunguzi wa ofisi jijini Arusha. Kwetu sisi uzinduzi huu unaonyesha nia namna gani tupo makini kuhudumia wateja wetu, ambao tunawapa kipaumbele. Tunaamini uwepo wa ofisi hii utaleta ushindani wenye manufaa sokoni na kusaidia kufikisha huduma kwenye sekta zilizoachwa nyuma na huduma za bima kama utalii, kilimo bishara na viwanda.

Tuna uhakika kuwa uwepo wetu hapa Arusha utakuwa na manufaa katika mkoa mzima na kwamba huduma zetu hapa zitakuwa na kuwa bora zaidi. Tutaendelea kujenga na kuimarisha ushirika thabiti kwa kutoa viwango vya juu vya malipo ya bima, huduma za ushauri wa majanga mbalimbali na kufupisha muda wa kulipa wateja

Sekta ya bima nchini imekuwa ikikua kwa asilimia 17.7 kwa mwaka, huku mapato ya bima yakipanda hadi kufikia Tsh 814.5bn kwa kipindi cha mwaka wa 2019-2020, kutoka mapato ya Tsh 691bn mwaka uliotangulia. Vilevile katika kipindi hicho,TIRA imesajili makampuni ya bima 31, madalali 10 na mawakala 780.

Kampuni ya Strategis inamilikiwa asilimia 100 na wazawa na wafanyakazi wake asilimia 100 wanatoka nchini humu. Mbali na ofisi iliyozinduliwa Arusha, kampuni hii ina ofisi nyingine Zanzibar na Dar es Salam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here