Home LOCAL JESHI LA POLISI LIMETOA MAFUNZO KWA MAFUNDI WA MAGARI

JESHI LA POLISI LIMETOA MAFUNZO KWA MAFUNDI WA MAGARI

Mkuu wa Usalama Barabarani  Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli Mbezi luis Dar es eslaam ASP Ibrahim Samwix  akizungumza na mafundi  wa magari waliyokuwa ndani ya Kituo cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi Luis, mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuwafundisha jinsi ya kutambua vifaa ambavyo vipo kwenye magari hayo.

Mafunzo hayo yametolewa leo Mei 29, 2021.

Na: Mwandishi Wetu.

JESHI la Polisi kitengo cha Usalama barabarani, limetoa mafunzo kwa mafundi magari waliyokuwa ndani ya Kituo cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi Luis, Dar es Salaam kwa lengo la kuwafundisha jinsi ya kutambua vifaa ambavyo vipo kwenye magari hayo.

Mafunzo hayo yametolewa leo Mei 29, 2021 na Mkuu wa Usalama Barabarani, ASP Ibrahim Samwix ,kwa lengo la msfundi hao kutambua mfumo wa injini ya gari unavyofanya kazi ili kuwaraisishia namna ya utengenezaji wa magari.

Pia,Mkuu huyo  aliwafundisha kuhusu kifaa cha aina ya turbo kinavyofanya kazi, na namna ya kukitambua kama kikiwa  kibovu, kwa sababu mafundi wengi wamekuwa wakifanya masuala ya ufundi kwa mazoea.

ASP Samwix alitoa pia mafunzo katika kifaa cha mfumo wa rejeta namna kinavyofanya kazi, kwa sababu mafundi wengi na madereva wamekuwa wakishindwa kutunza mabasi wanayopewa kutokana na mapungu madogo madogo.

Kabla ya mafunzo hayo, Mkuu huyo alianza na madereva kwa kuelimisha jinsi ya kufuata sheria za barabarani na kuendesha gari kwa mwendo ambao unatakiwa ili kuepusha ajali na kuokoa maisha ya wananchi.

Kwa wa upande wa madereva hao ambao walikuwa zaidi ya 40, walilishukuru Jeshi la Polisi kwa mafunzo hayo, kwa sababu yanawakumbusha kufuata sheria za barabarani, kutokana na kwamba wengi wanafanya kazi hiyo kwa mazoea.

Pia, wanasema ni mara yao ya kwanza kupatiwa mafunzo, kwa hiyowao wameona ni bahati kubwa kwa sababu wamejifunza mambo mengi kwa wakati mmoja kwa sababu wakati mwingine tunahisi kuwa tumesahaulika

Waneomba elimu hiyo na mafunzo hayo yawe endelevu kwa manufaa yao na kwa manufaa ya watumiaji wa barabara, wao wapo tayari muda wowote na pia wataendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.

Kwa upande wa abiria, Athuman Omary ambae ni Mkazi wa Tabata, Dar es Salaam alitoa shukrani kwa jeshi hilo kwa elimu ambayo walikuwa wanaitoa kwa dereva na wamiliki wa mabasi kwa sababu inaonesha ni jinsi gani wanajali maisha ya abiria.

Pia, Mkazi wa Ubungo, Mwajuma Juma aliwata madereva hao kutumia mafunzo waliyoyapa kwa kupunguza ajali za usalama barabarani kwa sababu kuna baadhi ya madereva hawafuati sheria hizo kwa makusudi.

Kwa upande wawamiliki wa mabasi, wamelipongeza jehi hilo kwa mafunzo ambayo wamepewa madereva wao pamoja na mafundi wa mabasi, wanasema hiyo itaondoa ajali za barabarani, itasaidia ulinzi wa magari yao na pia ushirikiano baina ya askari na wao utakuwa wa manufaa.

Previous articleMAGAZETI YA LEO J.MOSI MEI 29-2021
Next articleAFIIA WAADHIMIA KUFANYA KAZI KWA KUTUMIA VIWANGO VYA KIMATAIFA KATIKA KUFANYA KAGUZI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here