Home LOCAL HOSPITALI MIRACOLO SEGEREA KUPIMA AFYA BURE

HOSPITALI MIRACOLO SEGEREA KUPIMA AFYA BURE

NA:HERI SHAABAN, DAR ES SALAAM.
HOSPITALI ya Miracolo inatarajia kutoa matibabu ya afya bure kwa wakazi Jimbo la Segerea Wilayani Ilala siku ya Jumamosi Mei 29 mwaka huu 

Matibabu hayo ya afya bure kwa magonjwa mbalimbali yanatarajia kuanza SAA mbili asubuhi hadi SAA kumi jioni  kituo cha dalaadala Segerea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana
Mratibu wa shughuli hiyo Dkt.Bingwa wa Watoto wa hosipitalii ya Maracolo Anna Deogratias alisema nwaka 2021 Hospitali hiyo inadhimisha miaka mitano ya kutoa huduma kwa wananchi  katika madhimisho hayo wametenga siku hiyo kwa ajili ya kutoa matibabu bure kwa wakazi wa Jimbo la Segerea na maeneo ya jirani .

Dkt. Anna alisema baadhi ya magonjwa ambayo yatatibiwa siku hiyo nj presha,Kisukari,Wingi wa damu ,HIV,afya kinywa na meno na magonjwa nyemelezi .

Aidha Dkt ,Anna alisema pia watakuwepo wataalam Bingwa wa hospitali hiyo kwa ajili ya kutoa ushauri wa afya kwa wananchi watakaojitokeza kupewa matibabu .

Alisema kujua afya yako mapema ni muhimu wananchi wengi wamekuwa wakishindwa kuangalia afya zao kwa wakati hospitali ya Maracolo inaunga mkono juhudi za serikali katika kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ndani ya miaka mitano Hospitali ya MIRACOLO imepata mafanikio makubwa pia wameshirikiana na Serikali vizuri katika suala zima LA afya .

Mwisho
Previous articleMAGAZETI YA LEO J.NNE MEI 25-2021.
Next articleNAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII AWATAKA WAFANYAKAZI WA WIZARA HIYO KUONGEZA UBUNIFU.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here