Home LOCAL HAKUNA MACHINGA ATAKAEONDOLEWA WALA KUBUGUDHIWA DAR: RC KUNENGE.

HAKUNA MACHINGA ATAKAEONDOLEWA WALA KUBUGUDHIWA DAR: RC KUNENGE.

DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakar Kunenge amesema hakuna mfanyabiashara mdogomdogo almaarufu Kama Machinga atakaeondolewa Katika Jiji hilo Kama taarifa za uzushi kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii zinavyodai ambapo amawataka Wananchi kupuuzia taarifa hizo.

RC Kunenge amesema Serikali inatambua na kuthamini Mchango wa wamachinga kwenye Mkoa huo hivyo amewataka waendelee kufanya biashara zao kwa kufuata Sheria, kanuni na taratibu.

Aidha RC Kunenge amewataka machinga wasijenge kwenye mapito ya watembea kwa miguu Wala Barabarani kwani kwa kufanya hivyo wanahatarisha usalama wao na Vyombo vya Moto.

Pamoja na hayo RC Kunenge ametoa angalizo kwa Wafanyabiashara wenye utaratibu wa kubeba mitungi ya gesi na majiko yanayowaka na kukatizanayo katikati ya watu na Vyombo vya Moto Jambo ambalo ni hatari kwa kiusamama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here