Home BUSINESS ELIMU NA HAMASA ITOLEWE KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUHUSIANA NA BIMA.

ELIMU NA HAMASA ITOLEWE KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUHUSIANA NA BIMA.

Kaimu katibu tawala mkoa wa Arusha Agney Chitukuro akifungua maonesho na kampeni ya bima kwa wakulima na wafugaji.
Mmoja wa wakulima ambaye ameshanufaika na bima akiwaeleza wakulima wengne jinsi bima ya kilimo na bima ya afya zilivyomsaidia.
Mwakilishi wa  waandaji wa maonesho na kampeni ya bima kwa wakulima na wafugaji hayo Grace Kavishe akisoma risala yao.

Mwakilishi wa makapuni ya Bima Gasto Mrema alieleza namna makampuni hayo walivyojiandaa kuwafikia wakulima na wafugaji.

NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Kaimu katibu tawala mkoa wa Arusha Agney Chitukuro amesema kuwa suala la bima kwa wakulima na  wafugaji bado halijazoeleka hivyo inahitajika elimu na hamasa ili waweze kufahamu.

Chitukuro  aliyasema hayo wakati akifungua maonesho ya huduma ya bima kwa wakulima yaliyofanyika mkoani Arusha kwa udhamini WE EFFECT ambapo alisema ili kazi hiyo iwe na ufanisi watoe elimu na kwenda vijijini lakini pia washirikiane na serikali.

“Hapa kuna watoa huduma kumi na tatu na wengi wanagusa kuwafikia wakulima na wafugaji lakini niiombe TIRA kuendelea kuwqhamsisha watoa huduma za bima wengi zaidi kulifikia kundi hili na ili kupata manufaa na uelewa ni lazima waende vijijini,” Alisema Chitukuro.

Aidha aliwataka wakulima na wafugaji kutumia fursa ya maonesho hayo kujifunza na kujiunga na bima lakini pia wahusika kuhakikisha wanatoa urasimu na mlolongo mrefu wa upatikanaji wa huduma za bima.

Mwakilishi wa  waandaji wa maonesho hayo Grace Kavishe alisema kuwa  maonesho hayo yamepewa kauli mbiu isemayo“kilimo bora na uhakika wa bima” ambao umelenga kuhamasisha huduma Bora na ufikiwaji wa huduma za bima kwa wakulima na wafugaji katika ukanda wa Kaskazini pamoja na Tanzania nzima kwa ujumla.

Alisema kuwa bima inafahami kuwa ni moka ya mfumo ya usalama kwa jamii za wakulima na wafugaji na hasa masikini wanaotegemea shughuli za kilimo na ufungaji hivyo bima imebaki kuwa moja ya muhimbili mikuu kwaajili ya maendeleo katika nyanja tofauti tofauti katika jamii.

Alifafanua kuwa licha ya wakulima na wafugaji kuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na usalama wa chakula katika taifa upatikanaji na ufikiwaji wa huduma bora za bima zimebaki kuwa changamoto ukilingalisha na jamii za wafanyabiashara ambao kwao upatikanaji wa huduma hizo zenye mgawanyiko unaendana  na biashara zao.

“Hii ni tofauti na kwa wakulima wanaotegemea cha misimu ya mvua zinazobadilika badilika kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kama ilivyoshuhudiwa kwenye miaka ya hivi karibuni,”Alisema Grace Kavishe.

Alifafanua katika kushughulikia suala la upatikaji wa bima shirika la kimataifa la WE EFFECT pamoja na wadau wake MVIWAKI, benki ya Mwanga  hakika,MVIWAARUSHA,na benki ya biashara ya Uchumi(UCB) wameandaa kampeni hiyo ili kuhamasisha wakulima na wafugaji na jamii kwa ujumla  hasa akina mama na vijana wanafikiwa na wakapata huduma bora za bima.

Kwa upande wa hutuba ya Shedrac  Otieno  kutoka WE EFFECT iliyosomwa na Damian Joseph alisema kuwa asilimia 80 ya chakula kinazalishwa na wakulima lakini wakulima wengi hawapati huduma ya bima ambapo taasisi hiyo inajitahidi kuhakikisha wanapata bima ili kumaliza umasikini.

Alisema kuwa chini ya asilimia tano tu ya wakulima ndio wanapata huduma za bima nchini ambapo ni kutokana uelewa mdogo, mazingira magumu ya kuzifikia huduma hizo pamoja na gharama kubwa na mchakato mrefu wakati wa kutafuta bima hizo.

“Tunaamini kupitia bima wakulima na wafugaji wa chini wataweza kufikia ili iweze kuwasadia katika kuwekeza zaidi na kumaliza umasikini.

Naye  mwakilishi wa makapuni ya Bima Gasto Mrema alisema kuwa wapo katika maonesho hayo ili kuweza kutoa  elimu kwa wakulima lengo likiwa ni kuhakikisha mkulima na mfugaji hawabaki nyuma kwa sababu Kuna mwamvuli wa bima unaweza kuwasadia kufanya shughuli zao bila kuwa na wasiwasi wa kupata hasara.

“Tumejipanga kikamilifu kuhakikisha kilimo cha kisasa na ufungaji wa kisasa unaendelea kutokana na bima kwani bima tunazozitoa zinawanufaisha pale changamoto zinapotokea,” Alisema Mrema.

Naye mmoja wa wakulima ambaye ameshanufaika na bima kutoka benki ya Uchumi Mike Ngowi kutoka Kilimanjaro alisema kuwa kupitia bima amepata mkopo wakuendeleza kilimo na kwa sasa anafanya uzalishaji kwa kujiamini kwani haofii kupata hasara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here