Picha ya Maktaba (Waziri wa Maliasili na utalii) Dkt. Damas Ndumbaro. |
NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Waziri wa maliasili na utalii Dkt Damas Ndumbaro amewasisistiza wafanyakazi wa wizara hiyo kuzingatia sheria, kanuni na miongozo katika kusimamia ukusanyaji wa maduhuli na ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
Dkt Ndumbaro alitoa rai hiyo katika hutuba yake ya kufungua mkutano wa 28 wa baraza la wafanyakazi wa wizara ya maliasili na utalii iliyosomwa na katibu mkuu wa wizara hiyo Dkt Allan Kijazi ambaye pia ndio mwenyekiti wa baraza hilo ambapo alisema kuwa suala la ukusanyaji wa maduhuli ni suala muhimu kwa wizara kama inavyoelekezwa katika sheria kanuni na miongozo mbalimbali ya serikali.
Dkt Kijazi alisema wanapaswa kukuza wigo wa bidhaa za utalii ili kufikia watalii milioni 5 i na kuongeza mapato kufikia dola za kimarekani bilioni 6 ifikapo mwaka 2025 ambapo ili kufikia azma hiyo wanapaswa kuimarisha utalii wa wa uwindaji wanyama pori, kukuza utalii wa mikutano pamoja na kuendeleza utalii wa fukwe.
Alieleza kuwa pia wanapaswa kuimarisha usimamizi, ulinzi na uhifadhi wa maliasili kwa faida yakizazi cha sasa na kizazi kijacho kwa kuendelea kujenga uwezo wa wa wadau katika kusimamia rasilimali za wanyapori,misitu na nyuki pamoja na kuendelea kudhibitib ujangili wa wanyama pori na na mazao ya misitu na nyuki kwa kuweka mazingira wezeshi ya kuvutia uwekezaji katika sekta .
“Lakini pia tunatakiwa kuendelea kusimamia, kuendeleza na kulinda malikale kwa manufaa ya taifa kwa kuboresha usimamizi, matumizi na uhifadhi wa maeneo ya malikale na urithi wa utamaduni ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu wezeshi ya utalii katika maeneo hayo kwa kuweka mazingira ya kuvutia wawekezaji na kuhamasisha kufanyika kwa matamasha ya kitamaduni,” Alisema Dkt Kijazi kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo Dkt Ndumbaro.
Aidha alisema kuwa wizara hiyo imeanzisha Jeshi la uhifadhi la wanayama pori na misitu kwa lengola kuendelea kulinda, kusimamia na kuhifadhi rasilimali hizo ambapo pamoja na hayo pia jeshi hilolinalenga kuimarisha nidhamu kwa watumishi na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku .
“Ninawaomba muendelee kuimarisha nidhamu, ukakamavu na uadilifu katika kutekeleza majukumu yenu ya uhifadhi na nimatumaini yangu kuwa matukio ya ujangili na biashara haramu ya mazao ya wanyapori na misitu yatapungua kwa kiasi kikubwa kutokana na jitihada zinazoendelea kufanya na Jeshi letu la uhifadhi wwanayam apori na misitu,” Alisema.
Sambamaba na hayo pia alieleza kuwa serikali inatoa kipaumbele katika kuboresha maslahi ya watumishi ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ya msingi kwa ufanisi unatarajiwa na wananchi ambapo serikali imetoa kibali cha kuwapandisha vyeo watumishi wenye utendaji mzuri na waliotengewa nafasi katika mwaka wa fedha 2018/2019 na 2020/2021.
“ Nina agiza wizara na wakuu wa Taasisis zote zilizo chini ya wizara ya maliasili na utalii kuwapandisha vyeo kabla ya nei 31 watumishi wote wanaostahili pamoja na kuendelea kuwapa mafunzo ya muda mfupi na mrefu ili kuweza kuwajengea uwezo na weledi utakao wawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi unaotarajiwa,” Aliagiza.
Kwa upande wake Lucius Mwenda mkurugenzi wa idara ya utawala na rasilimali watu waliyoyasikia katika mkutano huo yatawasaidia kujua mwajiri anataka nini na ni nini kimepangwa na wao watahusika katika kutekeleza ambapo kwa asilimia kubwa inategemea mwajiri kuwapa vitendea kazi, kujali maslahi ya wafanyakazi pamoja na utayari wa wafanyakazi.
Naye mwenyekiti wa chama cja wafanyakazi {TUGHE} tawi la maliasili na utalii Antony Tibaijuka alieleza kuwa wamepewa nafasi ya kupitia bajeti pamoja na kupewaruhusa ya kuzunguza yale waliyonayo jambo ambalo litawafanya wafanyakazi kutekelezamajukumu yao vizuri na kufikia malengo yanayo hitajika.