Home BUSINESS BRELA YAWATAKA WABUNIFU KUSAJILI VUMBUZI ZAO.

BRELA YAWATAKA WABUNIFU KUSAJILI VUMBUZI ZAO.

Afisa Mwandamizi- Utumishi na Utawala kutoka Idara ya Miliki Ubunifu BRELA, Bw Raphael Mtalima akifafanua juu ya sifa za Uvumbuzi unaoweza kusajiliwa kama Hataza kupitia BRELA wakati wa mashindano ya MAKISATU yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. BRELA inawakaribisha kutembelea kwenye banda lake katika mashindano ya MAKISATU yaliyoanza tarehe 6 hadi 11 Mei, 2021

DODOMA.

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni  (Brela)imewataka wabunifu na Wavumbuzi wa Sayansi na Teknoloijia kwenda Brela kusajili bunifu zao ili kuzipa Ulinzi na kulindwa kisheria.

Aidha Brela pia imewataka wabunifu hao kurasimisha Biashara zao ili waingie katika mfumo rasmi wa kutambulika Kitaifa na Kimataifa.

Hayo yalisemwa na Afisa Utumishi na Utawala anayehusika na maombi ya Ataza,alama za Biashara na huduma BRELA Bw. Raphael Mtalima   katika maonesho ya Mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Bunifu (MAKISATU) yanayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.

“Niwatake Hawa wabunifu na wavumbuzi walinde vumbuzi zao kwa kuzisajili Brela, hii itamsaidia kutambulika ndani na nje hata akiitaji mkopo kwaajili ya kuendeleza Biashara yake inakuwa rahisi”, alisema Afisa Mtalima.

Aidha Mtalima aliongeza kuwa vumbuzi,Bunifu na teknolojia  mbalimbali za Kisayansi Brela ndio Taasisi inayosismamia  Sheria ya Ataza, alama za Biashara na huduma hivyo inawajibu wa kutoa kwa wajasiriamali.

“Ni lazima wabunifu hawa wafaidike na Bunifu zao kwani wanatumia pesa nyingi kufanya tafiti zao hivyo ili kuweka Ulinzi wa hizo Bunifu zao ikiwa ni njia Kuu za kuwafaidisha kisheria” alisema Mtalima.

Aidha Afisa huyo wa Brela pia amewataka wakazi wa Dodoma na Vitongoji vyake kutumia maonesho hayo kwenda kusajili Biashara zao kwani huduma zinapatikana hapohapo Uwanjani.

Vilevile Mtalema alisema kuwa huduma za Brela pia zinapatikana kwa njia ya mtandao hivyo popote Tanzania huduma hizo zinapatikana.

Mashindano na maonesho hayo ya MAKISATU yaliyoanza Mei 6 hadi 11 mwaka huu na yamejumuisha zaidi ya wabunifu100..

Previous articleMWONGOZO WA UWEKEZAJI WA MKOA WA TABORA WAZINDULIWA.
Next articlePROFESA MDOE AWAKARIBISHA WATANZANIA KUJIFUNZA MBINU BORA ZA KILIMO BANDA LA TARI DODOMA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here