Home LOCAL TANZANIA NA SC Johnson ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA KUPAMBANA NA MALARIA

TANZANIA NA SC Johnson ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA KUPAMBANA NA MALARIA

Na.WAF, Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Aprili 2,2023 amesaini hati ya makubaliano ya kushirikiana na Kampuni ya SCJohnson ya nchini Marekani katika kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini.

Tukio hilo limehudhuriwa na Makamu wa Rais Mtendaji wa Shirika hilo Bw. Mark Martin, Balozi wa Umoja wa Viongozi wa nchi za Afrika dhidi ya Malaria (ALMA) Mhe. Anthony Okara pamoja na Mwenyekiti Mteule wa Baraza la Kutokomeza Malaria Tanzania Mhandisi Leodgar Tenga.

Tamko hilo limefikiwa kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan aliyoifanya kwenye makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Racine, Winscosin nchini Marekani mwezi Mei, 2022.

#MtuNiAfya
#JaliAfyaYako

Previous articleYANGA SC YAICHAPA TP MAZEMBE 1-0 KWAKO
Next articleRAIS SAMIA AFANYA UHAMISHO WA VITUO VYA MABALOZI, AFANYA UTEUZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here