Home SPORTS WATUMISHI BRELA WAIPA ‘SUPPORT’ SIMBA SC, WAFIKA KWA MKAPA KUISHANGILIA

WATUMISHI BRELA WAIPA ‘SUPPORT’ SIMBA SC, WAFIKA KWA MKAPA KUISHANGILIA

Shabiki wa timu wa simba Bw. Amon Peter Kayuni akifurahi pamoja na watumishi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), ambao wamehudhuria katika pambano la Kimataifa, Kombe la Klabu Bingwa Afrika (CAF), kati ya timu ya Simba na Horoya kutoka Guinea, leo tarehe 18 Machi, 2023 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam.

Watumishi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) leo wameunganga na mashabiki wa timu ya wekundu wa Msimbazi Simba SC kuishangilia timu hiyo katika mchezo wao wa Kombe la Mabingwa Afrika uliochezwa katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo timu ya Simba SC iliibuka na ushindi kwa kuichapa Horoya FC  jumla ya magoli 7-0 na kujihakikishia kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa kushika nafasi ya 2  ikiwa na alama 9, nyuma ya Raja Casablanca yenye alama 13.

Wakiwa katika uwanja wa Mkapa watumishi wa BRELA walionekana muda wote kuiunga mkono timu hiyo kwa kushangilia katika dakika zote za mchezo huo.

Uwepo wa Taasisi hiyo kushudia mtanange huo, ni hatua ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuunga mkono timu za Tanzania zilizofanikiwa kucheza hatua ya Makundi ya michuano ya CAF ambapo leo Simba SC imefuzu rasmi kutinga hatua ya robo fainali.

Previous articleSIMBA SC YAOGELEA MINOTI YA MAMA, YAIFUMUA HOROYA FC 7-0 KWA MKAPA
Next articleCde, KILUPI – AONYESHA NIA YA KUISAIDIA SKULI YA BUBUBU ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here