Home SPORTS SIMBA QUEENS, YANGA PRINCESS KUUMANA MACHI 22

SIMBA QUEENS, YANGA PRINCESS KUUMANA MACHI 22

Na: Tima Sultan 

WATANI wa jadi Simba Queens na Yanga Princess wanatarajia kushuka dimbani Machi 22 kuonyeshana ubabe kwenye Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Light Tanzania Bara.

Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini, Dar es Salaam Saa 10:00 jioni.

Akizungumza na wandishi wa Habari jana, Kocha Mkuu wa Simba Queens, Charles Lukula, alisema pamoja na kwamba wanaongoza msimamo wa ligi hiyo, lakini watacheza kama ndio mchezo wao wa mwisho.

Amesema wanaifahamu Yanga na wanajua katika kila mchezo ambao wanakutana nao changamoto huwa kubwa lakini wao wanahitaji ushindi hilo ndio kubwa ambalo wamejipanga nalo.

Kwa upande wa kikosi cha Yanga, Kocha Msaidizi wa timu hiyo Fredi Mbuna, amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mchezo huo.

Amesisitiza kuwa wamesharekebisha makosa yao ya nyuma na wataingia katika mchezo huo wakiwa na ari pamoja na morali ya kutosha ukizingatia wanapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa mashabiki wao

Previous articleTASAC YATOA MAFUNZO KUKABILIANA NA UMWAGAJI WA MAFUTA BAHARINI
Next articleRAIS SAMIA AIPONGEZA TADB, ASISITIZA KUENDELEA KUWEZESHA MIRADI YA BBT
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here