Home LOCAL ASKARI WA UHIFADHI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

ASKARI WA UHIFADHI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka Askari wa Uhifadhi katika maeneo mbalimbali nchini wazingatie sheria kanuni,taratibu na miongozo pindi wanapotekeleza majukumu yao ikiwemo kulinda Maliasili.

Ameyasema hayo leo Wilayani Ushetu Mkoani Shinyanga mara baada ya kutembelea Kata ya Mlowa wakati wa ziara yake kikazi yenye lengo la kutatua changamoto baina ya wananchi na wahifadhi.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inataka wananchi wake waishi kwa amani bila taharuki ya aina yoyote, hivyo Askari wa Uhifadhi wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya sheria.

“Sisi tumepewa dhamana ya kusimamia maliasili kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo, katika kutekeleza jukumu hili hatupaswi kuleta taharuki kwa wananchi” amesisitiza Mhe. Mary Masanja.

Amewaeleza wananchi hao kuwa mtu yeyote anapovunja sheria kwa kuingia katika maeneo yaliyohifadhiwa bila vibali lazima utaratibu wa kisheria ufuatwe ikiwemo kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Aidha, ametoa rai kwa wananchi hao waendelee kufuata sheria na kuacha kuvamia maeneo yaliyohifadhiwa kwa kuwa maeneo hayo ni muhimu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Pia, amewataka Askari Uhifadhi waandae programu za kutoa elimu kwa wananchi ili wajue umuhimu na faida za uhifadhi ikiwemo kuleta mvua, kutunza vyanzo vya maji,kuchavusha mazao na kusaidia katika masuala ya ulinzi na usalama wa nchi.

Naye,Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Mboni Mhita amesema ataendelea kushirikiana na wahifadhi kuhakikisha elimu ya uhifadhi inaendela kutolewa kwa wananchi wanaozunguka Pori hilo.

Previous articleZAO LA MPIRA KUENDELEZWA MAENEO YENYE HALI  YA HEWA INAUYOKUBALIKA NCHINI 
Next articleBARRICK NORTH MARA YAWA MWENYEJI WA KIKAO CHA TAIFA CHA SHIMMUTA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here