Home LOCAL MAHAKAMA ISIFUNGWE NA SHERIA YA HABARI – MEENA

MAHAKAMA ISIFUNGWE NA SHERIA YA HABARI – MEENA

MAHAKAMA haipaswi kufungwa na sheria ya habari katika kutoa hukumu yake kulingana na uzito wa kosa alilotenda mwandishi wa habari.

Sio sawa mahakama kulazimishwa na sheria kumfunga mwandishi miaka mitatu ama zaidi hata pale kosa lake linaweza kumalizwa kwa kuonywa ama kifungo chini ya miaka hiyo.

Ni kauli ya Neville Meema, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), leo tarehe 29 Agosti 2022, wakati akizungumza katika Kipindi cha Sun Down kinachorushwa na Radio Ukweli (Ukweli FM), Mjini Mrorogoro.

Amesema, baadhi ya vipengele vya Sheria ya Habari ya Mwaka 2016, vinailazimisha mahakama kutenda kwa matakwa ya watungaji wa sheria hiyo.

“Tusitunge sheria kwa ajali ya kuilazimisha mahakama kutenda kwa mujibu wa yaliyopo mioyoni mwa watunga sheria,” amesema Meena.

Akifafanua kauli yake amasema, hatua ya sheria kumuelekeza hakimu kutoa kifungo kisichopungua miaka mitatu, ni kumlazimisha asitoe hukumu chini ya kiwango hicho.

“Inawezekana hakimu akaona kosa la mwandishi linahitaji kifungo cha miaka miwili au mmoja au miezi sita na pengine miezi mitatu ama kifungo cha nje.

“Lakini kutokana na sheria hii, hakimu hawezi kutoa kifungo nje ya kile kilichoelezwa na sheria, sasa huku ni kulazimisha kila aliyetenda kosa kwenye tasnia ya habari afungwe sio chini ya miaka mitatu. Jambo hili tunaona lina ukakasi,” amesema Meena.

Previous articleSHAKA AIPONGEZA SERIKALI, DIT KWA UWEKEZAJI KWENYE GESI ASILIA KATIKA MAGARI
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 30-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here