Home INTERNATIONAL RAIS WA (IPU DKT. TULIA AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI MKUTANO WA MASPIKA...

RAIS WA (IPU DKT. TULIA AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI MKUTANO WA MASPIKA DUNIANI

New York
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameongoza Kikao cha Kamati ya Maandalizi cha Mkutano wa 6 wa Maspika Duniani, unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai 2025 mjini Geneva, Uswisi.

Mkutano huo umefanyika leo tarehe 12 Februari, 2025 katika ukumbi wa Umoja wa Mataifa (UN), uliopo Jijini New York, Marekani huku ukihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa IPU, Maspika, Manaibu Spika na Wakuu wa Misafara wa Mabunge ya China, Uingereza, Nigeria, Spain, Bahamas,Malta, Azerbaijan, Ivory Coast, Mexico, Uswisi, Algeria, Malawi, Canada na Qatar.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!