Home Uncategorized WASIRA KUTOA HOTUBA YA KISAYANSI JIJINI MWANZA

WASIRA KUTOA HOTUBA YA KISAYANSI JIJINI MWANZA

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Stephen Wasira 
Na Hellen Mtereko,Mwanza, Fullsgangwe Blog 
Wananchi wa Mkoa wa Mwanza na mikoa jirani wameombwa kujitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg.Stephen Wasira utakaofanyika Jijini Mwanza.
Hayo yamebainishwa Leo Februari 10, 2025 na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza Omary Mtuwa wakati akizungumza na Fullshangwe Blog ambapo amesema kuwa  mkutano huo utafanyika kesho Februari 11 mwaka huu katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini hapa.
Amesema Mkutano huo utakuwa wa kihistoria kutokana na kuwa na wasemaji wazuri watakao ongelea sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na hotuba ya kisayansi itakayotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho.
“Tumepata bahati ya kutembelewa na Stephen Wasira na ameingia leo Februari 10  tutampokea katika Wilaya ya Magu na baada ya kusalimia wananchi wa wilaya hiyo ataenda kuwasalimia wananchi wa kisesa kisha ataingia Mwanza kwa maandalizi ya Mkutano wa kesho”, amesema Wasira