Home LOCAL WATENDAJI KATA NA VIJIJI SONGEA WAONYWA KUACHA UPENDELEO MCHAKATO WA KUWAPATA WAHUDUMU...

WATENDAJI KATA NA VIJIJI SONGEA WAONYWA KUACHA UPENDELEO MCHAKATO WA KUWAPATA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma  Elizabeth Gumbo akiwa katika picha ya pamoja  na Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji na Wasimamizi wa Vituo vya kutolea Huduma za Afya  baada ya kupata mafunzo kuhusu Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii  yaliyofanyika Shule ya Sekondari Maposeni  Kata ya Peramiho, Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma  Elizabeth Gumbo akizungumza  na Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji na Wasimamizi vya Vituo vya kutolea Huduma za Afya  baada ya kupata mafunzo kuhusu Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii  yaliyofanyika  Shule ya Sekondari Maposeni  Kata ya Peramiho, Halmashauri ya Wilaya ya Songea    Ukumbi wa Jenista Joakim Mhagama  Hall .

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma  Elizabeth Gumbo akiwa katika picha ya pamoja na uwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa baada ya kufika Ofisi kwake katika zoezi la mafunzo ya Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji  na Wasimamizi wa Vituo vya kutolea Huduma za Afya katika Halmashauri hiyo Kuhusu Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.

………..

Na. Elimu ya Afya kwa Umma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma  Elizabeth Gumbo ametoa onyo kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kuacha Upendeleo katika mchakato wa kuwapata Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.

Gumbo ametoa onyo hilo katika Ufunguzi wa Mafunzo elekezi ya Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii  kwa Maafisa Watendaji wa Kata 16,Maafisa  Watendaji wa Vijiji 56 na Wasimamizi wa Vituo vya Huduma za Afya 45 wa Halmashauri hiyo yaliyofanyika  Shule ya Sekondari Maposeni  Kata ya Peramiho, Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jenista Joakim  Mhagama  Hall  .

“Mhudumu wa Afya Ngazi ya Jamii anayeomba yeye maombi ndiye anayefanya kwa ufanisi, Watendaji wa Kata na vjiji acheni upendeleo kwa kuleta watu wenu”

Aidha, Mkurugenzi huyo wa Halmashauri amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wana mchango Mkubwa katika Jamii.

“Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ni muhimu kwa Sababu wao ndio kiungo cha Serikali pamoja na jamii na wanarahisisha kufikisha Elimu ya Afya haraka ,mfano Elimu ya Lishe na chanjo na wanaongea lugha moja na wananchi  kwani wanatoka kwenye maeneo ya jamii husika”amesema.

Kwa upande wao baadhi ya Maafisa Watendaji akiwemo   Rajab Tamimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Parangu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Maafisa Watendaji  wa Kata katika Halmashauri ya Songea pamoja  Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Peramiho B  Rehema Nombo  wamesema kupitia mafunzo hayo itawarahisishia usimamizi uchaguzi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii huku wakiipongeza Serikali kwa kuja na Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika Mkoa wa Ruvuma. Jumla ya Watumishi 117 wamepata Mafunzo hayo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Previous articleWIZARA YA AFYA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALIMBALI WA MAENDELEO
Next articleSTAMICO KUANZA USAMBAZAJI WA NISHATI SAFI YA RAFIKI BRIQUETTES ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here