Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe Akizungumza na hadhara kwenye uzinduzi Maalum wa Nembo ya Taifa ya Viungo kwenye Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. |
Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.
Wizara ya VIWANDA na Biashara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Nchini (TanTrade) imezindua nembo maalum ya Taifa ya Viungo katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia katika uzinduzi huo Naibu Waziri Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amesema kuwa Nembo hiyo imeanzishwa rasmi ili kukuza Biashara za wajasiriamali na wafanyabiashara wa kitanzania wanaojishughulisha na Viungo ili kuweza kutambulika kwenye soko la ndani na nje.
Amewataka wadau wote kushirikiana ili kuweza kuleta tija na ufanisi mkubwa kwenye bidhaa hizo za viungo ambazo zimetokea kupendwa na kutumika na watu wengi wakiwemo raia wa kigeni.
“Serikali inataka kuona Sekta Binafsi inakuwa mwekezaji kinara hapa Nchini hii ni kutokana wananchi wengi zaidi ya 60 kujiajiri kwenye Sekta ya Kilimo hivyo tunaamini kwa kuwepo wa Nembo hii itazidisha amasa kwa wakulima wa Viungo kuongeza uzalishaji. Amesema.
Ameongeza kwa kusema kuwa Nchi ya Tanzania ina aina zaidi ya 30 y Viungo nakwamba Serikali imjikita kuendeleza aina tano za viungo hivyo ambavyo ni Karafuu, Mdalasini, Iriki, Piliipili manga na
Iriki kwakuwa mazao hayo huwa yakifanya vizuri kwenye Soko la ndani na nje ya Nchi.
Amesisitiza kuwa Nembo hiyo ya Taifa ya Viungo itumiwe vizuri hasa kuhakikisha Bidhaa za Viungo zibatangazwa vizuri kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha Bidhaa hizo zinafanya vizuri zaidi kimauzo.