Mwonekano wa wa baadhi ya wananchi wa kata ya Mapinga wilayani Bagamoyo wakati wa ziara hiyo.
(Mmoja wa bibi kikongwe ambaye alihudhuliwa katika mkutano huo akitoa kilio chake kwa Waziri wa ardhi nyumba maendeleo na makazi wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Bagamoyo. (PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
NA: VICTOR MASANGU,BAGAMOYO
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameagiza. watu watano akiwemo Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mapinga Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani kukamatwa mara moja kutokana na kuhusika na tuhuma za kuwafanyanyia vitendo vya utapeli kes kuwauzia maeneo wananchi kinyemela na kusababisha hali ya kuibuka kwa migogoro kila kukicha.
Lukuvi ametoa agizo la kukamatwa kwa watuhumiwa hao wakati wa ziara yake ya kikazi ambayo alifanya mkutano wa adhara na wananchi wa kata ya mapinga ambapo aliamua kuwaita watuhumiwa hao ambao wameonekana kutajwa zaidi katika kufanya vitendo vya utapeli na kuliagiza jeshi la polisi Wilaya ya Bagamoyo kuwakamata na kuwaweka ndani kwa ajili ya uchunguzi.
Aidha katika mkutano huo ambao ulihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali katika ngazi za Wilaya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambapo waziri alionekana kuchukizwa kabisa na vitendo hivyo vya utapeli kwa baadhi ya watu hao na wengine wakiwa ni viongozi wa chama na ndio akiwa katika mkutano huo akaamua watuhumiwa hao washikiliwe na polisi mbele ya umati ya wananchi ambao walifurika katika mkutano huo.
Watuhumiwa hao ambao Waziri aliamuru kukamatwa na polisi pamoja ni Omari Shabani ambaye ni Katibu Muenezi wa kata ya Mapinga, Ramadhani Rashidi aliyekuwa katibu wa kitongoji cha Kiembeni, Marwa Muhoni, William Urio na Mwanahamis Habibu
Lukuvi alimuagiza mkuu wa Polisi wilaya ya Bagamoyo kufanya mahojiano ya kina na watuhumiwa hao na wakibainika hatua za kisheria zichukuliwe kukomesha migogoro ya ardhi.
Pamoja na wananchi kuwataja watuhumiwa hao pia Diwani wa kata ya Mapinga Chandika Dismas pamoja na baadhi ya viongozi walikiri kiongozi huyo wa Chama auwa na jopo lake ambalo linashiriki kuuza maeneo na kuchochea migogoro katika eneo hilo.
Pia Waziri Lukuvi alisema kwamba lengo la serikali awamu ya sita ni kuhakikisha kwamba wanamaliza changamoto ya migogoro ya ardhi na kwamba wataweza mpango mzuri ambao utaweza kuwasaidia wananchi kuwapa elimu zaidi katika ngazi mbali mbali ili kuepukana na matapeli ambao wamekuwa wakijipatia fedha kwa njia isiyo ya halali.
“Katika Wilaya ya Bagamoyo imekuwa na chanagmoto kubwa sana ya migogoro ya ardhi ambayo ukichunguza zaidi inasababishwa na baadhi ya watendaji wa vijiji, na mingine inasababisha na viongozi kwa hiyo jambo hili mimi siwezi kulivumilia hivyo nitahakikisha kwamba suala la uvamizi wa maeneo tunalikomoseha kabisa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakari Kunenge amesema kwamba atahakikisha kwamba maaagizo yote ambayo yametolewa na Waziri atayafanyia kazi kwa misingi ya kuwachukulia hatua kazli za kisheria kwa wale wote amabo watabainika na kujihusiha na vitendo vya utapeli.
Kadhalika Kunenge aliwataka wanachi wote wa Mkoa wa Pwani kuachana kabisa na tabia ya kujichukulia maeneo kiholela na badala yake wahakikishe wanazingatia sheria na taratibu zote ili kuepukana na wimbi la migogoro ambalo limekuwa likisababishwa na baadhi ya watu.